HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 31, 2019

BENKI YA CRDB YAJIVUNIA FAIDA YA BILIONI 92


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 

Na Mwandishi Wetu 

ENKI ya CRDB imetengeneza faida ya Sh. Bilioni 92 baada ya kodi kati ya Januari na Septemba, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema hayo ni mafanikio makubwa ikilinganishwa na faida ya Sh. Bilioni 52 baada ya kodi iliyopatikana kipindi kam hicho mwaka 2018.

Alisema hayo ni mafanikio makubwa kwa benki hiyo yanayoashiria kukua, kuaminika na kuongoza kwenye sekta ya kibenki.

"Faida hii ya sh. Bilioni 97 no sawa na asilimia 76 ya matarajio ya malengo yetu na hii inatokana na utendaji mzuri wenye weledi wa watendaji wetu, wateja na zaidi ni ubora wa usimamizi wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki yetu," alisema Nsekela.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, faida hiyo imechangiwa na riba itokanayo na mikopo kwa asilimia 22 na huduma za kawaida kwa asilimia 13.

Aliwataka wanahisa wa benki hiyo kufurahia mafanikio hayo muhimu kwa kuwa nao watapata gawio kubwa baada ya pato la kila mwanahisa kuongezeka kutoka sh. 26 hadi sh. 41 huku akiwataka watanzania zaidi kununua hisia za benki ya CRDB.

Alisema kuongezeka kwa wateja, amana zao na riba za mikopo ndio siri ya mafanikio ya benki hiyo.

Alisema amana za wateja zimekua kwa asilimia saba hadi kufikia sh. trilioni 4.8 na kwamba mikopo imeongezeka kwa wafanyabiashara wakubwa na wajasiriamali.

Kwa upande wa mikopo, alisema ukuaji umekua mkubwa kwa wateja , wa kati na wajasiriamali huku akibainisha urejeshaji bora wa mikopo.

Kuhusu ajira, alisema kwa kipindi cha Januari hadi Septemba, mwaka huu benki hiyo imeweza kuongeza wafanyakazi kutoka 3,112 hadi 3,393 sawa na ongezeko la wafanyakazi zaidi ya 200.

Kwa upande wa wa raslimali za benki, Nsekela alisema zimekuwa hadi kufikia sh. trilioni 6.2 na kwamba kwa mwendo huo, wanaamini wataendelea kufanya vizuri zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages