Kaimu Ofisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (katikati), akimuonesha Mkurugenzi wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla, jinsi ya kulipia kwa Tigo Pesa Mastercard QR, wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Malipo, Mshana Mshana. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo kwa kushirikiana na Mastercard wamezindua kampeni kwa ajili ya kuwazawadia wateja wanaofanya malipo kwa njia ya Tigo Pesa Mastercard QR.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo Kaimu Mkuu wa Huduma za Fedha (MFS), Angelica Pesha alisema. “Kama kampuni ya kidigitali siku zote tunalenga kuleta sulushisho na kufanya maisha ya wateja wetu kuwa rahisi zaidi.
Kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa njia mpya na salama ya malipo kwa wateja pale wanapotaka huduma na bidhaa kwenye maduka na maeneo mengine ya kibiashara yanayoruhusu mfumo wa Mastercard QR," alisema.
Alisema katika maduka na maeneo yanayoruhusu kulipa kwa Mastercard QR kampeni hiyo imelenga katika kuhakikisha wateja wanapata huduma rahisi na ya uhakika nchi nzima.
Aliongeza, “Tigo Pesa Mastercard QR ni fursa ya kuchochea agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwa sababu Tigo Pesa ni huduma kamili ya kifedha.
Pesha alisema kupitia Tigo Pesa Mastercard QR si tu wanapanua wigo wa utoaji wa huduma zenye usalama kwa wateja bali wanasogeza huduma zenye uharaka karibu na wateja wetu.
Alisema baada ya malipo, mteja atapokea zawadi ya hadi asilimia 3 ya fedha kulingana na kiwango cha malipo aliyofanya.
"Mastercard QR ni njia ya haraka na ya kidigitali yakufanya malipo ambayo kwa sasa inakubalika katika maeneo mbalimbali ya kibiashara kwa wateja wote wa Tigo Pesa," alisisitiza Pesha.
Mkurugenzi na Meneja wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla alisema Mastercard imejizatiti katika kutafuta njia mbadala ya kifedha kwa kuja na suluhisho linatoa nafasi kwa wateja kupata huduma za malipo zenye usalama na za uhakika.
"Shabaha hii ya kuleta mbadala wa fedha ni jambo la kujivunia hasa tunapoungana na Tigo.
Aliongeza “Kwa sasa biashara nyingi zinapokea malipo ya Mastercard QR ambapo wateja wanaweza kutumia njia hii ya kidigitali kujipatia zawadi ya fedha kwa malipo waliyofanya.
"Mteja wa Tigo anaweza kufanya malipo kwa njia ya Mastecard QR kupitia App ya Tigo Pesa kwa kuscani QR. lakini ni dhahiri kuwa sasa Tigo Pesa ni ya kimataifa," alisema.

No comments:
Post a Comment