HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 24, 2019

BENKI YA CRDB YAKABIDHI GAWIO LA SHILINGI BILIONI 7.2 KWA RAIS DKT. MAGUFULI

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio kwa Serikali kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma. Wengine pichani ni Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa fedha Dkt. Philip Mpango.

Na Kilo Mgaya, Dodoma

Benki ya CRDB imekabidhi gawio la shilingi bilioni 7.2 kwa Serikali baada ya kupata matokeo mazuri ya kifedha katika mwaka wa fedha unaoishia Desemba 2018. Gawio hilo limekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Abdulmajid Nsekela.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kupokea gawio na michango kwa Serikali iliyofanyika Ikulu, Chamwino Dodoma, Rais Magufuli amepongeza mashirika na taasisi mbalimbali ikiwemo Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa na manufaa kwa Watanzania kupitia gawio linalotokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali.
"Taasisi nyengine zijifunze kutoka kwenu, tunahitaji kuona Watanzania wananufaika na uwekezaji wao kwani fedha hizi ndio tunakwenda kujenga reli, barara pamoja na ujenzi wa hospitali na vituo vya afya, nawapongeza sana," alisema Rais Magufuli.

Wachambuzi wa masuala ya fedha wanatazamia Benki ya CRDB kutoa gawio kubwa zaidi mwakani kwa Wanahisa wake ikiwamo Serikali baada ya kupata matokeo mazuri zaidi mwaka huu 2019 ambapo katika matokeo ya fedha ya nusu ya tatu ya mwaka benki hiyo iliripoti faida ya jumla ya shilingi bilioni 92.16 ukilinganisha na shilingi bilioni 52.25 zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Akizungumza baada ya hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela alisema matokeo mazuri ya kifedha ambayo benki hiyo imeyapata mwaka huu yanatokana na maboresho na uwekezaji katika mifumo ya kidijitali uliolenga kuongeza urahisi kwa wateja kupata huduma popote walipo jambo lililosaidia kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wateja.

"Tumehakikisha tunaboresha njia zetu mbadala za utoaji huduma kama SimBanking, SimAccount, Internet Banking, CRDB Wakala, Mashine za manunuzi (PoS), pamoja na kuunganisha mifumo yetu na mfumo wa malipo wa Serikali GePG, hii imerahisisha wateja kujihudumia wenyewe kwa kufanya miamala pale walipo," alisema Nsekela.

Nsekela alisema huduma hizo za kidijitali za Benki ya CRDB zimesaidia sana kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki nchini hususani vijijini. “Sasa hivi tuna CRDB Wakala zaidi ya 15,000 ambao wamesambaa nchi nzima,” aliongezea Nsekela.

Serikali imewekeza ndani ya Benki ya CRDB kupitia mfuko wa ushirikiano na Serikali ya Denmark (DANIDA), Mifuko ya uhifadhi wa jamii ya PSSSF, NSSF, ZSSF na GEPF, Mfuko wa Bima ya afya (NHIF), Mfuko wa Maendeleo wa Lindi, Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakifurahi jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako, wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakifurahi jambo na Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akizungumza na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichele, wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange, wakati wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Ally Laay. 
Afisa Mkuu Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshakanabo akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa, wakati  wa hafla ya upokeaji gawio na michango kwa serikali iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma. 


No comments:

Post a Comment

Pages