HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2019

KILIMANJARO QUEENS USO KWA MACHO NA KENYA FAINALI YA CECAFA 2019

Mshambuliaji wa Kilimanjaro Queens, Mwanahamis Omary 'Gaucho' akiwania mpira na beki wa Uganda katika mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya CECAFA. (Picha na TFF).
Mashabiki wakifuatilia pambano la Nusu Fainali ya michuano ya CECAFA kati ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Queens' na Uganda.

Na Mwandishi Wetu

MWENDO ni uleule, Kikosi  Cha timu ya taifa ya wanawake Tanzania 'Kilimanjaro Queens' kimetinga hatua ya fainali michuano ya CECAFA baada ya kuwanyuka Uganda bao 1-0 katika mtanange wa nusu fainali uliounguruma Dimba la Chamazi.

Mchezo huo ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili kwani zimefanikiwa kutengeneza nafasi nyingi lakini umakini wa kuweka mpira nyavuni ulidhibitiwa na safu za ulinzi kwa pande zote.

Bao la Tanzania limefungwa dakika ya 90 na nahodha,  Asha Mwalala ambaye alipokea mpira wa krosi  uliopigwa na Mwanahamisi Omari 'Gaucho' .

Tanzania itamenyana na Kenya kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa kwenye dimba hilo Jumatatu Novemba 25, ukitanguliwa na kandanda la kusaka mshindi wa tatu kati ya Uganda dhidi ya Burundi.

Mchezo mwingine wa nusu fainali uliochezwa kwenye dimba hilo, Kenya waliibuka kidedea dhidi ya Burundi kwa mabao 5-0.

Kwaupende mwingi  timu ya Kenya imeonekana kufurahia kucheza fainali na Tanzania wakiamini niwakati muafaka kwao kuonyesha uwezo wao kwa kuifunga timu hiyo.

Kama Kilimanjaro Queens wanafanikiwa kutwaa ubingwa huo itakuwa ni mara ya tatu mtawalia wakibeba Kombe hilo la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

No comments:

Post a Comment

Pages