Napenda kuwafahamisha kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama
Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, amewasimamisha kazi kuanzia leo tarehe
23/11/2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP RICHARD GEORGE ABWAO na RCO Mkoa wa Shinyanga SSP JOHN NDIBALEMA RWAMULEMA ili
kupisha uchunguzi.
Sababu za kusimamishwa kwao kazi ni kutokana na kushirikiana
na Wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha CANON cha mkoani
Shinyanga kukwepa kulipa kodi.
Sababu ya Pili ni Utovu wa Nidhamu kwa kushindwa kutekeleza maelekezo waliyopewa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni
Mkuu wa Mkoa huo Mhe, Zainab Telack.
Imetolewa na:
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania
No comments:
Post a Comment