Na Tiganya Vincent
SERIKALI
imewataka wadau kuunganisha nguvu zao pamoja katika kukabiliana na uharibifu wa misitu ya miombo ili
kulinda uoto wa asili na kuwa na mistu endelevu kwa ajili ya maendeleo ya ukuaji
wa uchumi nchini.
Kauli hiyo imetolewa
leo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa ufunguzi wa
warsha ya wadau wa ukanda wa miombo wa Mradi wa Usimamizi
shirikishi wa Misitu ya Miombo ya nyanda kame Tanzania.
Alisema pamoja na jitihada zinazofanywa
na Serikali na wadau bado kuna kiwango kikubwa cha uharibifu wa mistu ikiwemo ile
ya miombo na kusababisha kuwepo na tisho linaloweza kupelekea upotevu wa uoto
wa asili.
Makungu alisema uharibifu wa mistu usipothibitwa
utasababisha kuwa na gharama kubwa ya kurejesha uoto wa asili uliopotea na
wakati mwingine kusababisha kizazi kijacho kushindwa kupata matunda ya mistu iliyoharibiwa.
Alisema Mradi huu wa Uhifadhi wa Misitu ya
miombo katika nyanda kame umekuja wakati muafaka ambapo kila wadau wanatakiwa
wajiwekee malengo ya pamoja ili kutekeleza Mkakati wa Kuondoa uharibifu wa
ardhi na kukabiliana mabadiliko ya
tabianchi.
Naye
Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula Duniani
(FAO) nchini Jonathan Sawaya alisema
takwimu zinaonyesha kuwa uharibifu wa mistu hapa nchini ulifikia hekta 469,420
kwa mwaka 2018.
Alisema
hali inasababishwa na kuwepo na jitihada kubwa katika kupunguza uharibifu wa
mistu na ardhi unaotokana na shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabia
nchi.
No comments:
Post a Comment