Mfano wa kahawa iliyolimwa na kuwekewa mbolea na madawa yenye kemikali za viwandani ambazo ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
Baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea shamba la Mkulima Remmy Temba wa Kijiji cha Shimbwe Juu kata ya Uru Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro kujionea namna ya kulima bila kuweka mbolea na dawa za viwandani zinazopata rusha maisha ya walaji.
Na Irene Mark, Moshi
WAFANYABIASHARA wa Kahawa inayolimwa bila kemikali, kutoka Uingereza na Afrika Kusini wamesema uhitaji wa kahawa hiyo ni mkubwa duniani kuliko upatikanaji wake.
Wafanyabiasha hao walitembelea shamba la mkulima Remmy Temba anayelima mazao mbalimbali kwa njia ya asili katika Kijiji cha Shimbwe Juu, Kata ya Uru mkoni Kilimanjaro.
Walisema wanalazimika kutembelea mashamba ya wakulima wa kahawa halisi ili kujiridhisha na mazingira ya ulimaji bora wa zao hilo muhimu kwa afya na uchumi.
Paul Cooker toka Kampuni ya CTCS ya England alisema mahitaji ya kahawa inayolimwa kwa njia za asili ni makubwa na bei yake ipo juu.
"Tunaamini kahawa hii ni bora na upatikanaji wake umekuwa adimu sana... hii kahawa isiyo na kemikali ni tiba pia huondoa msongo wa mawazo na maumivu ya kichwa," alisema Cooker.
Mfanyabiashara Mart Carter kutoka kampuni ya Tribeca Coffee ya Africa Kusini alisema dunia inahitaji kurudi kwenye uasili wake hivyo ni muhimu kuhamasisha pia ulaji wa vyakula visivyozalishwa kwa kemikali za viwandani.
"...Mazingira haya ni mazuri na kikubwa watu wanatakiwa kurudi kwenye uasili wao kama ilivyo mandhari hii," alisema Carter.
Mkulima Temba alisema wakulima wengi wanatumia mbolea na madawa yenye kemikali za viwandani ambazo ni hatari kwa afya ya binaadam.
"Hiki kihamba ni eka tatu nimerithi toka kwa baba yangu na baada ya kupata elimu kuhusu ukulima wa asili miaka 15 iliyopita nikaamua nami kulima bila mbolea na dawa za viwandani.
"Ni kilimo kizuri kwanza kinakupa amani na mazao yake ni asili kabisa tunaishi tukiwa na afya njema... bei ya vyakula vya asili iko juu na wanaoelewa wananunua kwa pesa nyingi," alisema Temba.
Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Emmanuel Kiahule, alisema matumizi ya vyakula visivyozalishwa kwa kemikali yanampunguzia mlaji hatari ya kupata maradhi yasiyoambukizwa.

No comments:
Post a Comment