Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, wakati aliwasili kwenye Msikiti
wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambao ameufungua
rasmi, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Abdallah Ulega, wakati aliwasili kwenye Msikiti wa Haq Kionga,
uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambao ameufungua rasmi, Novemba
29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Sheikh Hamid Jongo,
kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar
es Salaam, kabla ya kuufungua rasmi, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu).
Sheik Jongo, akizungumza na Waumini wa Kiislamu, kwenye ufunguzi wa
Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba
29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Waumini wa Kiislamu,
kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar
es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waumini wa Kiislamu, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia
kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar
es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kufungua rasmi, Msikiti wa
Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati akifungua
rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam,
Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiingia msikitini, baada ya kufungua
rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam,
Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisikiliza mawaidha kwenye swala ya
Ijumaa, baada ya kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo
Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema madhehebu ya dini yametoa mchango mkubwa katika
kuwapata viongozi wa Serikali wanaofuata maadili mema na miiko ya uongozi.
Akizungumza wakati
alipofungua Msikiti wa Haq – Kionga ulioko Magomeni, jijini Dar es Salaam leo
mchana (Ijumaa, Novemba 29, 2019), Mheshimiwa Majaliwa amesema imedhihirika
kwamba waumini wazuri wa dini mbalimbali wamebainika kuwa ni viongozi wazuri na
waadilifu ndani ya Serikali.
Amewasihi
viongozi wa dini waendelee kuwafundisha maadili mema waumini wao ili Taifa liendelee
kuwa na raia wema ambao baadhi yao ndiyo watakakuwa viongozi katika
ngazi mbalimbali hapo baadaye.
“Nyumba za ibada
ndiyo mahali sahihi panapojengwa maadili mema kwa watu wa rika zote, hivyo
nawaomba Watanzania wawe waumini wazuri wa dini zao kwani kwa kufanya
hivyo watakuwa pia ni raia wema,” amesema Mheshimiwa Majaliwa.
Amesema wazazi
na walezi wanawajibika kuwarithisha watoto wao imani za dini vizuri kwani
anaamini kwa kufanya hivyo watoto watajengewa misingi mizuri ya imani ya dini na
maadili mema na watakapokuwa watu wazima watakuwa ni raia wema.
Mheshimiwa
Majaliwa aliwasilisha mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Magufuli wa sh. milioni 10 na yeye pia alichangia sh. milioni tano ili
zisaidie katika awamu ya pili ujenzi wa msikiti huo.
Naye Sheikh Masoud Jongo ambaye alimwakilisha Sheikh Mkuu
wa Tanzania katika ufunguzi wa msikiti huo, alisema uhuru mkubwa wa kuabudu uliopo
nchini ndiyo sababu kubwa inayoifanya Tanzania iwe ni nchi ya amani
na utulivu.
Sheikh Jongo
amewaomba Watanzania wautumie vizuri uhuru mkubwa wa kuabudu uliopo nchini kwani
ni nchi chache duniani zinazotoa uhuru mkubwa wa kuabudu kwa wananchi wake kama
ilivyo hapa Tanzania.
No comments:
Post a Comment