HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 05, 2019

Utafiti wabaini kuku wanaouzwa wakidaiwa ni wa kienyeji si wa kienyeji

NA JANETH JOVIN

UTAFITI uliyofanywa na Shirika linalohusika na usalama wa wanyama duniani (World Animal Protection) umebaini kuwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji si wa kienyeji kama inavyosemwa.

Utafiti huo umebaini kuku hao si wa kienyeji bali ni kuku wa kisasa maarufu kama kuku wa kizungu wanaofungwa majumbani kwa kupewa majani pamoja  na dawa mbalimbali za kuwakuza na kuwafanya kuwa wanene.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, Msemaji Mkuu wa Shirika hilo, Victor Yamo alisema utafiti huo ambao ulifanywa Juni hadi Julai mwaka huu katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam umebaini jambo hilo hivyo watumiaji wanapaswa kuwa makini.

Yamo anasema kuku wengi wanauzwa katika mikoa hiyo wamekuwa wakupewa dawa za kuwakuza  ambazo zina madhara kwa binadamu pindi wanapotafuna mifupo ya kuku hao.

"Wakati watu wetu wakitembelea kwenye masoko mbalimbali kuulizia bei ya kuku na aina walibaini uwepo wa kuku wa kisasa wengi na mwananchi uuziwa kwa kuambia kuwa ni wa kienyeji jambo ambalo ni uongo," anasema

Anasema utafiti huo ulifanyika kwa lengo la kujua walaji wananunua nyama za aina gani, kutoka wapi pamoja na  kuangalia kama wanafahamu ubora wa chakula na matumizi ya dawa za wanyama.

"Tunaamini kuwa mteja ataelewa nyama anayotaka kununua au kula inaubora au tatizo kiasi gani, hiyo itakuwa rahisi kujiepusha nayo na kutafuta kitu kingine mbadala cha kula," anasema

Aidha Yamo anasema kwa sasa Shirika lao linafanya jitihada kubwa kuhakikisha linaimarisha ustawi na haki za wanyama na sheria za kuwalinda wanyama hao zinapitishwa na serikali husika katika kila nchi.

Anasema pamoja na kuyafanya hao wanatoa wito kwa watanzania waanze kuelewa kuwa kama watashindwa kuangalia ustawi wa wanyama hasa wanaoliwa kuna hatari kubwa ya kupotea.

"Ni ukweli uliyowazi kuwa ustawi wa wanyama ni muhimu sana na kwa kutambua hilo tumekuwa tukienda mashuleni kufundisha jambo hilo na masuala ya usalama wa chakula pamoja na ubora wa dawa," anasema.

No comments:

Post a Comment

Pages