Meneja
wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (wa pili toka kulia)
akikabidhi msaada huo wa vifaa vya ujenzi ikiwemo bati vyenye thamani ya
Sh. Milioni 20/= kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida
Paskasi Mlagiri, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule
ya msingi Misuna na Msange, pia zahanati za vijiji vya Mwachambia na
Mwakichenche, wilayani Singida.
Meneja wa Benki ya NMB
Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (kulia), akivikwa shuka maarufu kama ‘mgolole’
kutoka kwa mwanamke wa jamii ya Kinyaturu mkazi wa kijiji cha Msange,
ikiwa ni ishara ya upendo kwa benki hiyo kwa
mchango wake kwenye sekta ya elimu wilayani Singida.
KERO ya kusoma mazingira yasio mazuri kwa wanafunzi zaidi ya 350, wakiwemo wasichana 169 wa kitongoji cha Misuna, kijiji cha Ngimu wilayani Singida, imepatiwa ufumbuzi baada ya jamii kwa kushirikiana na benki ya NMB kujenga miundombinu ya vyumba vya madarasa.
Wananchi
hao wameshirikiana na Benki ya NMB kumaliza kero hiyo, kutokana na
watoto wao kupata usumbufu wa kutembea mwendo mrefu kila siku kwenda
shule na kurudi nyumbani huku mchana kutwa wakilazimika
kushinda na njaa.
Wakipokea
msaada wa vifaa mbalimbali kutoka Benki ya NMB, baadhi ya wananchi
walisema kuwa, kila siku watoto wao walilazimika kutembea mwendo wa
kilomita tano kwenda shuleni, na zingine tano kurudi
nyumbani, hali iliyozorotesha taaluma yao.
Akikabidhi
baadhi ya vifaa hivyo ikiwemo bati, mbao, nondo, misumari, makoa na
waya kwa ajili ya ujenzi, meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati yenye
mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara; Nsolo Mlozi,
alisema Benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi.
“Benki ya
NMB itaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha changamoto
zote zinazoikabili jamii zinatatuliwa, kipaumbele chetu ni kwenye sekta
za elimu na afya"alisema.
Meneja
huyo alifafanua kuwa, msaada huo wenye thamani ya Sh. Milioni 20/=, kwa
ajili ya shule mbili za msingi na zahanati mbili, ni mwendelezo wa benki
hiyo katika kuhakikisha inarejesha faida
inayopata, kwa jamii ili itumike kuleta maendeleo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Paskasi Mlagiri, alisema kuwa msaada
katika shule hiyo ya Misuna na mingine iliyotolewa kwenye shule ya
msingi Msange, zahanati ya kijiji cha Mwakichenche
na Mwachambia, ni chachu kwa jamii katika kujiletea maendeleo yao.
Hata hivyo
Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi kuendelea kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao, ikiwemo ujenzi wa matundu ya
vyoo, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu,
madawati na zahanati.
Aidha
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Eliya Dighah, kwa niaba
ya wananchi wa wilaya hiyo,aliishukuru Benki ya NMB kuwekeza kiwango
kikubwa cha fedha za maendeleo katika halmashauri
hiyo, hali inayojenga imani kwa jamii.
#NMB Karibu Yako
No comments:
Post a Comment