HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2020

WANANCHI WATAKIWA KUZIUNGA MKONO TAASISI ZISISO ZA KISERIKALI

 Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga (kulia), akiwa na Mhifadhi anayesimamia Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara, Noelia Myonga (kushoto) katika Tamasha la Siku nne la Fursa lililofanyika hivi karibuni Uwanja wa Mazingira Bora wilayani Karatu. Tamasha hilo liliandaliwa na TAMUFO kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo.Katikati ni Mwimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha.
 Viongozi waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii. Kutoka kushoto waliokaa ni  Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) , Dkt. Donald Kisanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza na Mwanamuziki Mzee Kingkii na walio simama kutoka kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo, John Shaban, Mwimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha, Msanii Rajab Samata kutoka kundi la muziki wa dansi na wa tano ni Katibu wa TAMUFO,  Stella Joel na Mwimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone na wa nne ni mdau wa muziki aliyefahamika kwa jina moja la Flora.
 Wananchi wakiwa kwenye tamasha hilo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza, akiserebuka kwenye tamasha hilo.
 Viongozi wakiwa meza kuu. Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu,   Theresia Mahongo. 

Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Karatu mkoani Manyara  Theresia Mahongo amewata wananchi kutoa ushirikiano kwa Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali kama ya Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) zenye nia nzuri ya kuhamasisha maendeleo katika jamii kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali.
Mahongo ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa ombi hilo wakati akihutubia kwenye Tamasha la Fursa la siku nne lililofanyika wilayani humo ambalo liliandaliwa na TAMUFO kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo.
" Nawaombeni wananchi jengeni tabia za kuzipa ushirikiano taasisi kama hii ya TAMUFO ambazo zinakuja kuhamasisha maendeleo katika wilaya na mkoa wetu" alisema Mahongo.
Katika hatua nyingine Mahongo alitumia tamasha hilo kuwaeleza  wananchi umuhimu wa kutunza mazingira na kupiga vita vitendo vya rushwa na kusisitiza kuhusu amani na utulivu kwa ajili ya nchi yetu.
Rais wa TAMUFO Dkt.Donald. Kisanga akizungumzia tamasha hilo lililofanyika Uwanja wa Mazingira Bora wilayani humo alisema lililenga kuhamasisha mambo mbalimbali katika Jamii hasa kuunga mkono juhudi za Serikali.
Katibu wa TAMUFO Stella Joel alisema tamasha hilo lilipambwa  na waimbaji kutoka sehemu mbalimbali kama vile Upendo Nkone,  Emmanuel Mbasha,  John Shabani Pamoja na Mzee Kingkii 
na wengine wengi.
Alisema mbali ya wanamuziki hao pia walikuwepo madaktari kutoka Wilaya ya Karatu ambao walitoa vipimo na elimu ya afya bure na maofisa kutoka Damu Salama ambapo watu mbalimbali walichangia damu na lita 80 zilipatikana.
Joel aliongeza kuwa katika Tamasha hilo maofisa wa Basata na Cosota walikuwepo kusajili vikundi vya Sana na kumbi za starehe ili watambuliwe na Serikali.
Alisema tamasha hilo lilihitimishwa kwa maombi ya kuwaombea viongozi na nchi yetu na kuwa TAMUFO imekuwa  ikifanya matamasha kama hayo katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kutoa fursa hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages