Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Hassan Abbasi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020.
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
amesema kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dkt. Hassan Abbasi Said ataendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali .
Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam
katika hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliyowateua hivi karibuni.
Katika hafla hiyo Rais Magufuli alisisitiza kuwa kabla ya
uteuzi huo Dkt.Abbasi alipokuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji
Mkuu wa Serikali alifanya kazi nzuri ya kuisemea serikali kwa kushirikiana na
Waziri wa wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe na menejimenti.
“Ningependa aendelee kuwa msemaji wa Serikali lakini mahali
mtu anapotakiwa kupata promosheni kwa sababu ni Motivating Agent ndiyo maana
nimemteuwa kuwa
Katibu wa Wizara hiyo na kwa sasa hivi ataendelea kuwa
Msemaji wa Serikali mpaka tutakapo pata mwingine”alisema Mhe. Rais Magufuli.
Katika kipindi cha uongozi wake alitangaza miradi ya
Serikali, pamoja na kueleza utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayoendelea kufanyika
pamoja na kuanzisha
kipindi cha viongozi kusema utekelezaji wa majukumu ya
taasisi zao kupitia Kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na Televisheni ya TBC
1 katika mwaka mpya wa 2020 alianzisha kauli mbiu ya
TUMEAMUATUNATEKELEZA2020.
Aidha Viongozi wengine walioapishwa katika hafla hiyo ni
Makatibu Wakuu 05, Makatibu Tawala wa mikoa 03, Kamishina Jenerali wa Magereza
na Kamishna Jenerali
wa zimamoto na uokoaji, Kamishina wa ardhi Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Msajili wa
Mahakama ya Rufani,
Msajili wa Mahakama Kuu na wajumbe 03 wa Tume ya Utumishi wa
Mahakama.
No comments:
Post a Comment