HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 25, 2020

MFUMO WA UTOAJI LESENI ZA UDALALI WAZINDULIWA RASMI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (katikati) , akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salam katika uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Utoaji Leseni za Udalali na Waendeshaji minada. (Na Mpiga Picha Wetu).


Na Faraja Ezra

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James amezindua Mfumo wa Kielekroniki wa utoaji leseni za udalali na uendeshaji wa minada ambao utasaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Katibu huo alieleza kuwa Mfumo huo utaongeza ufanisi na tija katika kutekeleza majukumu  ya kiserikali ya uendeshaji wa minada  na utoaji wa leseni.

Pia alisema Wizara  imekuwa ukifanya jitihada kubwa katika ili kuboresha huduma hiyo, na kwamba kwa sasa huduma hiyo hupatikana kwa njia ya  compyuta na  simu ya kiganjani.

" Hakuna haja ya kupoteza muda kwa kusafiri wizarani kusajiliwa hivi sasa Wizara ya Fedha umeona kuwa hiyo ni changamoto hivyo, imeanzisha Mfumo huo wa Kielekroniki ili kuwarahisishia huduma wananchi wake" alisema Doto.

Aidha pia kutokana na ukuaji wa Sayansi na  teknolojia  hivi sasa Wizara imeona kuna umuhimu wa kuwa na mfumo huo ili kuondoa usumbufu kwa kufuatilia utoaji wa leseni ili kuendana na ulimwengu wa kisasa.

Pia kumekuwa na changamoto za waendesha minada na udalali kufanya kazi kinyume na sheria na wakati mwingine wanawarubuni watu jambo linaikosesha  serikali kipato hivyo Mfumo huo utasaidia kupunguza madalali feki.

Amewataka madali kuzingatia sheria iliyowekwa na Mamlaka husika na iwapo yeyote atakayepatikana akikiuka taratibu hizo anayeenda  kwa kweli hatuna huruma nao.  hatutasita kumchukulia hatua Kali za kinidhamu.

"Maana siku hizi wapo madalali feki wanaodanganya wananchi kuwa wana vibali halali vya kutoa leseni na wakati mwingine  kuwarubuni ili kukidhi mahitaji yao sasa kupitia Mfumo huu tutawafahamu madalali feki" alisema.

Alisema mfumo pia utawezesha kupata uhalali wa leseni kwa haraka na uwazi kwa kukomesha ufisadi na utarahisisha kazi.

Amewataka madalali kusajiliwa katika mfumo huo  kwa Mujibu wa sheria na kwamba kwa yeyote atakayekiuka sheria hiyo atachukuliwa hatua stakiki.

Doto alisema kuanzia leo maombi yote ya usajili yaataanza kupitia simu ya kiganjani na kompyuta.

No comments:

Post a Comment

Pages