HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2020

MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE AGUSWA NA MAFURIKO MANYONI

 Mwananchi wa Kijiji cha Kintinku akipeana mkono na Mhe Mbunge Aysharose Mattembe baada ya kukabidhi msaada wa maturubai kijijini hapo.
 Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni, ndugu Jumanne Makanda, Mbunge V/Maalum CCM mkoa wa Singida Aysharose Mattembe, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Daniel Mtuka na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kintinku, Patrick Anderson wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipowatembelea wahanga wa mafuriko Kijiji cha Kintinku.
 Mhe. Mbunge Aysharose Mattembe  akisalimiana na wananchi.
 Mbunge wa Viti  Maalum Mkoa wa Singida,  Aysharose Mattembe  akikabidhi msaada huo kwa viongozi mbalimbali. Kutoka  kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka,  Mkuu wa Wilaya ya Manyoni,  Rahabu Mwagisa na wa mwanzo kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Manyoni,  Abius Mligwa.
Wananchi wa Kijiji cha Kintinku waliokumbwa na mafuriko wakimsikiliza Mhe.Mbunge  Mattembe alipowatembelea  kijijini  hapo kuwapa pole.
 Msaada ukipokelewa.
Msafara wa magari ukipita kwenye maji wakati wa kutoa msaada huo.

Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose amewatembelea wahanga wa mafuriko wa kijiji cha Kintinku na Kitalalo wilayani Manyoni kwa lengo la kuwapa pole na kuwafariji pamoja na kuwachangia maturubai wahanga hao.
Mafuriko hayo yaliyotokea wiki iliyopita yameleta madhara makubwa na kusababisha  nyumba 2864 kudondoka na yameharibu miundombinu ya hospitali, shule, mashamba  barabara na madaraja .
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kintinku Mhe. Mattembe alisema "Nimeguswa na tukio hili lililoleta uharibifu wa makazi yenu na ninawapa pole sana enyi ndugu zangu, ninawaomba muwe watulivu katika kipindi  hiki kigumu kwenu kwani Serikali ya CCM ipo pamoja na nyie, nimekuja na msaada wa maturubai na ni matumaini yangu yatasaidia kwa kipindi hiki".
Aliongeza kusema, aliona ni vyema kununua maturubai ili wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo waweze kuyatumia kujikinga na mvua  na jua wakati mipango ya kupata makazi ya kudumu ikifanyika.
  
Akipokea msaada huo Mtendaji wa Kata ya Kintiku, Hadija Missanga alimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo
"Tunashukuru sana Mhe.Mattembe kwa msaada huu kwani wananchi wengi hawakuwa na sehemu ya kukaa baada ya nyumba zao kusombwa na maji hakika msaada huu ambao umeutoa leo hii umekuja kwa wakati" alisema Missanga.
Mbunge Mattembe alitumia pia nafasi hiyo kumpongeza  Mkuu wa Wilaya ya Manyoni,   Rahabu Mwagisa, Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki mhe.Daniel Mtuka, Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Manyoni, Kamati ya maafa ya wilaya pamoja na Benki ya NMB kwa ushirikiano mkubwa  walioutoa kuhakikisha mambo yanakaa sawa 
"Alisema nawapongeza sana viongozi wangu wa Chama na Serikali wa wilaya ya Manyoni na ninaipongeza na kuishukuru Benki ya NMB kwa kujitoa kwao mara kwa mara katika shughuli za kusaidia jamii kwa kweli wamekuwa mstari wa mbele nawapongeza sana" alisema Mattembe.
Katika msafara wa kwenda kuwapa pole waliokumbwa na mafuriko hayo Mbunge Mattembe aliongozana Mkuu  wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa,kamati ya maafa ya wilaya, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, mhe Daniel Mtuka, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Manyoni  Jumanne Makanda, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Charles Fusi, Diwani wa Kata ya Kintiku Gaspari Mgate, Afisa Mtendaji wa Kata Kintinku,  Hadija Missanga, Mwenyekiti wa  Kijiji cha Kintinku Patrick Anderson,  Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitalalo Mgomi Maganza na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Manyoni, Abius Mligwa na maafisa wa benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages