Mkurugenzi
wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi
wa usambazaji vitabu vya kiada darasa la 1 mpaka V kwa shule
zinazotumia lugha ya kingereza na vile maandishi ya nukta nundu darasa
la 1 mpaka 1V na kidato cha 1 mpaka IV.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akizungumza wakati
wa uzinduzi wa usambazaji vitabu vya kiada darasa la 1 mpaka V kwa
shule zinazotumia lugha ya kingereza na vile maandishi ya nukta nundu
darasa la 1 mpaka 1V na kidato cha 1 mpaka IV.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa usambazaji vitabu vya nukta nundu. Kulia ni mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la TET, Stanslaus Mpemba.
Baadhi ya wadu walioshiriki uzinduzi huo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika uzinduzi huo.
Tunazindua kwa pamoja.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa usambazaji vitabu vya kiada darasa la 1 mpaka V kwa
shule zinazotumia lugha ya kingereza na vile maandishi ya nukta nundu
darasa la 1 mpaka 1V na kidato cha 1 mpaka IV.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema kuwa haitegemei kuona vitabu ambavyo havina ithibati ya serikali na ikigundulika hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Hayo yalielezwa leo na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, wakati wa uzinduzi wa usambazaji vitabu vya kiada darasa la 1 mpaka V kwa shule zinazotumia lugha ya kingereza na vile maandishi ya nukta nundu darasa la 1 mpaka 1V na kidato cha 1 mpaka IV.
Ole Nasha amesema shule zote zitatumia vitabu vyenye ithibati ya serikali haijalishi shule ya medium au shule za serikali za kawaida.
"Shule zote zitumie vitabu vyenye ithibati ya serikali haijalishi wewe unatoka Atlas wala wapi,"
"Ukionekana unapindisha maagizo hayo basi sheria itachukua mkondo wake na vitabu hivi hakikisheni vinapelekwa mashuleni haraka tayari kwa kutumiwa uwiano ulioelekezwa,"alisema Olenasha.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TAET) Dk. Aneth Komba naye alikadhia kauli ya waziri na kutoa wito kwa wamiliki wa shule binafsi,wazazi na wadau wengine wa elimu kutumia vitabu vya kiada na ziada vilivyopata idhini ya serikali.
"Na niwaombe wasimamizi wa elimu wakiwemo wadhibiti ubora wa shule kusimama na kuhakikisha kuwa shule zinatumia vitabu sahihi na kwa idadi ya vitabu vilivyopo kwa sasa hakuna kabisa sababu ya kutumia vitabu ambavyo havina idhini ya serikali," alisema Dk.Komba.
Aliishukuru serikali pia kwa kutoa fedha zake kutoka mapato ya ndani na kufanikisha kazi ya uandishi na uchapaji wa jumla ya makala 1,305,950 vya English medium .wasioona nakala 38,200 kwa darasa la 1,11,V na kwa darasa la 111 ba 1V makala 14,904 kwa uwiano wa mtu mmoja mmoja.
No comments:
Post a Comment