WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
anatarajiwa kuwa na kikao na uongozi wa Riadha
pamoja na wadau wa mchezo huo kitakachofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro, Jumapili
Machi Mosi mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo, Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), linapenda
kuwaalika wadau wote wa mchezo wa Riadha wakiwamo makocha, waandaaji wa matukio
mbalimbali ya mbio (Race Organiser), kuhudhuria kikao hicho.
Kikao hicho muhimu, kitafanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro.
Ni mategemeo yetu RT, Wadau wengi wa mchezo wa Riadha watahudhuria bila
kukosa kwa manufaa ya mchezo wetu, hasa ikizingatiwa siku hiyo ni siku ya mbio
maarufu za Kilimanjaro Marathon.
IMETOLEWA
NA:
Tullo
Chambo
Msemaji RT
0752 46 21
03
27/02/2020
No comments:
Post a Comment