Afisa Mkuu wa Wateja Bianfsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Mhandisi Elius Mwakalinga kwenye hafla hiyo.
Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Biashara ya Serikali – Aziz Chacha akiongea kwenye Hafla iliyowakutanisha Benki ya NMB na Wakandarasi wa Kanda ya Ziwa jijini Mwanza. Pembeni yake ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi.
Mkuu wa Idara ya Huduma za Kifedha wa Benki ya NMB (NMB Head of Trade Finance Department) – Linda Teggisa (katikati) akitoa mada kwenye mdahalo kati ya NMB na Wakandarasi kutoka Kanda ya Ziwa kwenye Hafla hiyo.
5. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Mhandisi Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya Serikali kwenye mdahalo kati ya NMB na Wakandarasi kutoka Kanda ya Ziwa.
BENKI ya NMB mwaka jana imetoa zaidi ya dhamana 500 kwa wakandarasi wazawa ili kuwawezesha kugharimia miradi mbalimbali ya ujenzi nchini. Mkakati huo ulifikiwa kufuatia kilio cha muda mrefu cha wakandarasi kushindwa kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali kutokana na ukata wa fedha na ushindani toka kwa makampuni ya nje.
Akiongea wakati wa kongamano lililohudhuriwa na zaidi ya wanadarasi 300 kutoka Kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa NMB Filibert Mponzi alisema zoezi hilo litakua endelevu.
Alisema mbali na kusaidia kuwanyanyua wakandarasi wadogo kimtaji, pia Benki hiyo imeitikia wito wa Rais John Magufuli alioutoa juu ya taasisi mbalimbali za kibenki kuwakopesha wakandarasi kwa masharti nafuu.
“Kama benki ya biashara na kama mbia wa serikali tumeshiriki kikamilifu kuwasaidia wakandarasi kimtaji na pia kuitikia wito wa Rais Magufuli kuhakikisha kada hiyo inashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi,” alisema Mponzi.
Mkakati wa kutoa dhamana kwa wakandarasi umesaidia sana kuwawezesha kupata kazi za uhakika za ujenzi na kwa mujibu wa Mponzi benki inatoa dhamana ya asilimia 50 ya thamani ya mradi husika. Mbali na kutoa dhamana ya mikopo NMB pia itaanza kutoa huduma ya bima kwa waka ndarasi hao kuwawezesha kushiriki kwa ufanisi zaidi kwenye miradi mbalimbali kwa riba nafuu.
Hata hivyo, alisema wakati benki ikibuni njia mbalimbali za kuwasaidia wakandarasi wadogo na wazawa kuna umuhimu mkubwa kwao kuwa waaminifu katika urejeshaji wa mi kopo na kuheshimu masharti ya dhamana ili kuepuka kulipa riba kubwa kama adhabu baada ya mikataba kukiukwa.
Katika kongamano hilo lililohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eliud Mwakalinga wakandarasi walijadili chan gamoto mbalimbali na kushauri mikakati mbalimbali ya kupambana nazo.
Akizungumza nao, Katibu Mkuu Mwakalinga mbali na kuishukuru NMB kwa ubunifu na huduma za mikopo na dhamana kwa wakandarasi wazawa alisema kazi za ujenzi zinahitaji uaminifu mkubwa na kuzi ngatia ubora. Alisema tafiti mbalimbali zinaonesha wakandarasi wazawa hasa wadogo wamekuwa wakishindwa kupewa kazi kubwa kwa zababu kadhaa zikiwamo wengi kushindwa kuajiri wahandisi waliobobea na wenye weledi usiotiliwa shaka.
“Tumefanya utafiti na kugundu a kuna shida kubwa kwa wakandarasi wengi wadogo kushindwa kukaa na wahandisi waliobobea kwa kukwepa kuwalipa mishahara wanayostahili na kuishia kuajiri wahandisi wanafunzi na hata mafundi mchundo tu,” alisema.
Mhandisi Mwakalinga alidokeza mbinu kadhaa za kuwawezesha wakandarasi wadogo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanashindana katika kujenga miradi mikubwa inayoshikiriwa na makampuni mengi ya nje.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakandarasi Mkoani Mwanza Mhandisi Oscar Munishi aliwataka wakandarasi wazawa kujitathmini juu ya uadilifu wao kazini na kwamba kuna mapungufu kadhaa yanayohitaji kufanyiwa kazi miongoni mwao. Aliyashukuru mabenki yaliyojitokeza kuwadhamini kwa mikopo ya riba nafuu na akaishukuru NMB kwa kukutana nao na kujadili nao namna ya kuboresha utendaji kazi na kushindana kikamilifu sokoni.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment