Afisa Lishe Mkoa wa
Tabora Monica Yesaya akitoa maelezo mafupi jana kuhusu mambo muhimu
yanayohitaji katika masuala ya lishe wakati kikao cha tathimini ya nusu
mwaka ya mkataba wa lishe kwa ngazi ya Mkoa.
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema hatapitisha bajeti ya
Halmashauri itakayoshindwa kutenga shilingi 1,000/- kwa ajili ya kila mtoto
aliye chini ya miaka mitano kama ilivyoagizwa.
Alisema kila Halmashauri inatakiwa kupitia mapato yake ya ndani itenge
kiasi hicho cha fedha kila mwaka kulingana na idadi ya watoto waliopo katika
eneo lao.
Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua kikao cha tathimini ya nusu
mwaka ya mkataba wa lishe kwa ngazi ya Mkoa.
Alisema katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha ni vema kila Halmashauri
ihakikishe imetenga fedha hizo ili kukidhi matakwa ya mapambano dhidi ya
utapiamlo.
Mwanri alisisitiza kuwa Halmashauri ambayo haitaweka wazi mipango yake
haitapita wakati wa Kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) cha kupitia bajeti.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema masuala ya lishe lazima yawe ajenda ya
kudumu ya kuanzia ngazi za vijiji hadi Mkoa na kwenye nyumba za Ibada.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema asilimia 25.8
ya watoto mkoani humo wamedumaa na
hawana uwezo wa kufundishika na kuleta tija katika uchumi wa Taifa.
Aliwataka Maafisa wanahusika na mipango na bajeti kuhakikusha
wanashirikiana na Makatibu wa Afya na Maafisa Lishe kupanga mipango lishe
kwenye bajeti.
No comments:
Post a Comment