Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akizungumza na vikundi
vya wanawake wajisiriamali walijitokeza kuupokea msafara wa kijinsia wa
kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chamila amesema vitendo vya ukatili wa
kijinsia havitokei kwa wanawake pekee bali hata wanaume wanapigwa na
kunyanyaswa na wanawake.
Hayo
yamesemwa kwa niaba yake leo mkoani humo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya
Mhe. William Paul Ntinika alipokuwa akiupokea msafara wa kijinsia wa
kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mhe.
Ntinika amesema kuwa jamii imekuwa iikiweka nguvu katika kuwatetea
wanawake kwa kuwa wamekuwa wakitoa taarifa ya kufanyiwa vitendo vya
ukatili kwa wanawake hivyo nguvu pia inahitajika ya kutoa elimu kwa
wanaume ili waweze kutoa taarifa ya vitendo hivyo.
Ameongeza
kuwa Serikali inaendelea katika kupambana na vitendo vya ukatili wa
kijinsia hasa dhidi ya wanawake na watoto kwa kuanzisha mipango na Sera
mbalimbali zinazosaidia kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo katika mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
"Sisi
mkoa wa Mbeya tuko vizuri tunapambana na vitendo vya ukatili juzi tu
tulipata taarifa kutoka kwa mtoto kuwa anafanyiwa vitendo vya ukatili na
baba yake na tumeshamchukulia hatua za kisheria"alisema
Akizungumzia
malengo ya msafara wa kijinsia Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha amesema msafara huo umelenga
kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia katika
familia na jamii kwa ujumla.
"Kuelekea
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tumekuja na msafara wa kijinsia
ili tuweze kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu kupambana na vitendo vya
ukatili" alisema
Kwa
upande wake Balozi wa Kampeni ya Twende Pamoja Nurdin Bilal 'Shetta'
amesema suala la mapambano ya ukatili wa kijinsia ni suala la jamii yote
katika mapambano hayo hivyo wameungana na Serikali katika kuhakikisha
elimu inaifikia jamii ili kuondokana na vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment