NA GOODLUCK
HONGO
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk.Elikana
Kalumanga amesema uamuzi wa serikali wa kuwahamisha wanyamapori aina ya Simba
17 wa familia moja kwenda katika hifadhi mpya ya Buguri-Chato unapaswa kupongezwa.
Kauli hiyo
ilitoa jijini Dar es Salaam juzi na wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa
waandishi wa habari za mazingira yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa
Habari za Mazingira nchini (JET) kwa
kushirikiana na USAID PROTECT.
Mwezi
Februari mwaka huu,Serikali kupitia idara ya wanyamapori iliwasafirisha Simba
17 wa familia moja yakiwemo madume mawili kwa ajili ya kuwaweka katika hifadhi
mpya ya Chato-Bugiri mkoani Geita.
Akizungumzia
suala hilo alisema wanyama wanaishi kulingana na mazingira waliyoyazoea kama
walivyo viumbe wengine duniani hivyo kuchukua familia nzima ya Simba hao
kutawapa furaha katika makazi yao mapya ambayo itawasaidia kuendelea kuishi
hadi watakapozoea mazingira hayo mapya.
Alisema
wanyamapori kama Simba,Tembo na wengine huwa na tabia zao hivyo kuwahamisha
bila kufuata na kuzingatia mahitaji yao muhimu kunaweza kusababisha waishi wa
huzuni na wakati mwingine wanaweza kufa.
Dk.Elikana
Kalumanga ambaye ni mtaalamu wa sekta ya wanyamapori kutoka UDSM,alisema Simba
huwa na tabia ya kuishi pamoja kama familia ambapo kila baada ya mwaka mmoja
Simba dume hupigana na Simba mwenzake dume na atakayeshinda ndiye atayeendelea
kuishi na familia.
Alisema
ikiwa Simba dume mwenye familia anaweza kuuawa na mwenziwe basi hata watoto nao
wanaweza kuuawa wote ili Simba huyo mpya aweze kuwa na familia yake.
“Tunaipongeza
Serikali kwa uamuzi wa kuwahamisha Simba wa familia moja kutoka hifadhi ya
Serengeti hadi Chato-Bugiri kwa kuwa hata wanyama nao huwa na huzuni
wanaipoishi mbali na familia zao na wanaweza kufariki hivyo kuhamishwa kwao
kulifuata taratibu za kuwalinda wanyama hao”alisema Dk.Kalumanga
Alisema hata
Tembo huishi kwa familia moja miaka yao yote ambapo baadhi ya wanyama pia kama
digidigi ambao nao huishi pamoja kama familia lakini ikitokea mmoja kati ya mume
au mke akafariki basi aliyebaki ataishi peke yake hadi mwisho wa maisha yake.
“Wanyama
waliopo katika hifadhi ya Ruaha,Mikumi na Serengeti wanatofauti kutokana na
mazingira wanayoishi ambapo ukamataji wa wanyama unaofanywa na Simba katika
Mbuga ya Serengeti ni tofauti na ule wa Simba aliyeko Mikumi au Ruaha kutokana
ana uwepo wa misitu”alisema Dk.Kalumanga.
Katika
mafunzo hayo,waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipata
fursa ya kujifunza tabia za wanyamapori,ujangili,masoko ya nyara za wanyamapori,sheria
pamoja na utalii.
Mkurgenzi
Mtendaji wa JET John Chikomo alisema chama hicho kitaendelea kutoa mafunzo kwa
waandishi wa habari ili waliasaidie
taifa katika masuala la uhifadhi wakiwemo wanyamapori.
No comments:
Post a Comment