Meneja Mkuu wa kampuni ya Kusafirisha mafuta Kati ya Tanzania na Zambia
(TAZAMA) Abraham Saunyama akikabidhi vifaa vya Ujenzi vya mfumo wa Maji
kwa mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi wa ofisi ya Askari wa Usalama
barabarani kituo Cha Polisi Mikumi Christopher Magwai.
Na Ghisa Abby, Morogoro
KAMPUNI
ya Kusafirisha Mafuta kati ya Tanzania na Zambia(TAZAMA) Kanda ya
Tanzania, imekabidhi vifaa vya ujenzi vya mfumo wa maji kwa ofisi ya
Askari wa Usalama Barabarani Kituo cha Polisi Mikumi cha wilayani Kilosa
mkoani Morogoro.
Akikabidhi
vijaa hivyo leo, Meneja Mkuu wa TAZAMA Kanda ya Tanzanai, Abraham
Saunyama alisema Tanaka kama taasisi ya Serikali itaendelea
kushirikiana na jamii katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kusaidia kwenye mambo ua kimaendeleo kama ya kiuchumi.
Saunyama
alisema wao kama shirika pamoja na kufanyakazi ya kusafirika mafuta
wana jukumu la kusaidia jamii kwenye mambo mbalimbali, na wamekuwa
wakifanya hivyo maeneo bomba la mafuta linakopita.
Alisema
jeshi la polisi baada ya kutuma maombi Tazama ofisi hiyo waliona kutoa
vifaa vya ujenzi vya mfumo huo wa maji kwani pamoja na kukamilika kwa
ofisi huduma muhimu ni kuwepo kwa mfumo wa maji ili kuhakikisha jengo
hilo linakuwa salama na safi kwa watumiaji.
“Hii
ni taasisi ya Serikali tuna wajibu wa kusaidia na tunawahakikisha kuwa
tuko tayari kusaidia maeneo mengine hivyo msisite kutuambia,sisi ni
majirani kwa maana ya huu ni ujirani mwema,”alisema Saunyama.
Alisema Tazama itaendelea kusaidia kwenye maeneo mengine, ambapo aliomba kuendelea kushirikiana na kudumisha urafiki wao.
"Vifaa hivi vigharimu zaidi ya shilingi milioni 2 ni imani yetu vitatatua tatizo," alisema.
Aidha
alisema pamoja na kukabidhi vifaa hivyo wataangalia namna ya kusaidia
maeneo mengine ya kituo cha Polisi Mikumu kama eneo la mahabusu ili
wanapokuwa katika chumba wawe salama zaidi.
Mwenyekiti
Kamati ya Ujenzi wa Ofisi hiyo ya Askari Christopher Magwai, alisema
msaada huo ni muhimu na utasaidia kuwaweka askari katika mazingira
salama zaidi.
Magwai
alisema ujenzi wa ofisi hiyo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 28 na
hiyo ni michango ya wadau kwa kushirikiana na jeshi la polisi na kwa
asilimia 90 imekamilika baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo vya mfumo wa
maji.
Akisema kwa sasa
kilichobaki ni milango, samani pamoja na rangi hivyo ombi kwa wadau
kuendelea kuchangia ili ofisi hiyo iweze kuanza kutumika.
Mkuu
wa Kituo cha Polisi Mikumi (OCS) Anastazia Basagae, alisema kasi ya
ujenzi ilikuwa ikifanyika kwa kusuasua na sasa baada ya kukamilika ni
imani litatumika kwa lengo lililokusudiwa.
Alisema
katika jitihada za kuhakikisha linakamilika jengo wadau wameweza
kujitolea kwa kiasi kikubwa kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Akisema wanaomba wadau kutochoka kuchangia kwa kuwa kuna eneo la chumba cha mahabusu kutokuwa katika mazingira salama.
No comments:
Post a Comment