Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,
Mhandisi Zena Said na Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Leonard Masanja wakiwa
katika kikao na wadau mbalilimbali wa mafuta (hawapo pichani) kujadili hatua ambazo nchi itazichukua endapo uhaba wa
mafuta utajitokeza katika kipindi hiki cha Mripuko wa maradhi ya Virusi vya
Corona,jijini Dar es Saalam, Machi 17, 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said (aliyesimama),akizungumza
kwenye kikao baina Waziri wa Nishati na wadau mbalimbali
wa Mafuta nchini,jijini Dar es Salaam, Machi 17, 2020. Kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt
Medard Kalemani na kulia ni Naibu Katibu Mkuu
Mhandisi Leonard Masanja.
Wadau mbalimbali
wa mafuta nchini wakiwa katika kikao cha pamoja baina ya Waziri wa Nishati na wadau wa Mafuta
nchini, kilichofanyika ofisi za Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) jijini
Dar es Salaam,Machi 17, 2020.
Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani(aliyesimama) akizungumza na wadau wa mafuta nchini(hawapo
pichani) katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi za
Wakala wa Uagizaji Mafuta Kwa Pamoja ( PBPA) jijini Dar es Salaam, Machi
17,2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
Dustan Kitandula na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said.
Hafsa
Omar, Dar es Salaam
Waziri wa
Nishati, Dkt.Medard Kalemani, amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa mafuta nchini kujadili hatua ambazo nchi itazichukua
endapo uhaba wa mafuta utajitokeza katika kipindi hiki cha Mlipuko wa maradhi
ya Virusi vya Corona.
Tukio hilo
lilifanyika Machi 17, 2020 jijini Dar es Salaam, katika
ofisi za Wakala wa Uagizaji Mafuta Kwa Pamoja ( PBPA),na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara
ya Nishati Mhandisi Zena Said, Naibu Katibu Mkuu Mhandisi, Leonard
Masanja, Kamishina wa Petroli na Gesi Adam Zuber na viongozi mbalimbali wa Taaasi
za Wizara ya Nishati na wadau mbalimbali wa mafuta nchini.
Aidha,amesema
kuwa, Serikali imepanga kukutana na wadau hao ili kuona namna bora ya kuhakikisha
mafuta yatapatikana muda wote kulingana na mahitaji ya nchi, endapo itatokea
dharura yoyote kwenye nchi ambazo wafanyabiashara na wanaponunulia mafuta na
kuhakikisha kuwa shughuli zote zinaendelea nchini.
“ Sisi kama
Serikali pamoja na wadau ni jukumu letu kuhakikisha kwamba mafuta yanapatikana
muda wote tena ya kutosha kuendesha shughuli zenu wafanyabiashara lakini na
kuendesha shughuli za Serikali pamoja na shughuli za kijamii zote ziendelee kama
kawaida”. Alisema
Alisema,nchi inajenga
miradi mingi mikubwa ya kimaendeleo na kiasi kikubwa miradi hiyo inategemea sana
mafuta katika kuendesha shughuli za
uendeshaji.
Aliongeza kuwa,
nchi ambazo Tanzania inanunua mafuta, mpaka sasa bado wanaendelea na uzalishaji
wa mafuta na bado hawajafunga mipaka yao,lakini
kwa upande wa Serikali lazima ichukue hatua Madhubuti kwa kushirikiana wadau wake
ili kuweza kujiachia mafuta ya kutosha nchini.
Hata hivyo.Dkt
Kalemani amewatoa wasiwasi watanzania kwamba mafuta yapo ya kutosha ya hali ya
kawaida kabisa ambayo mpaka miezi miwili ijayo yatatosheleza, mafuta ya dizel,petroli
na mafuta ndege yote yanapatikana nchini na Serikali itajipanga zaidi ili kuwa na mafuta ya siku
nyingi zaidi.
Alifafanua kuwa,hata
kama nchi ina mafuta ya kutosha kwa kipindi hiki lakini Serikali haitakaa kimya
na kuona nchi inakosa mafuta ya kutosha kama Serikali lazima itafute kinga
badala ya kusubiri kuhangaika na tiba.
Waziri Kalemani,aliwashukuru
wadau hao wa mafuta kwa michango yao mizuri yenye uwazi na inayoangalia hali
halisi ya upatikanaji wa mafuta inavyoendelea nchini na kuwapongeza kwa kutoa
michango yenye tija ya kulisaidia Taifa endapo kama itatokea dharura yoyote katika
kipindi hiki cha maradhi Corona.
Nao, wadau wa
mafuta nchini, wameipongeza Serikali kwa kitendo cha kuwaita ili kuzungumzia suala
hilo ambalo limejikita katika kuchukua tahadhari ambazo zinajitokeza katika
kipindi ambacho dharura itayojitokeza na kuahidi kuwa wapo tayari kushirikiana na
Serikali ili kuhakikisha mafuta nchini yanapatikana muda wote.
Aidha walitoa
ushauri wa njia mbalimbali ambazo wanaziona zikichukuliwa zitasaidia katika
kukabiliana na uhaba wa mafuta kama hilo tatizo la uhaba litajitokeza siku za
mbeleni.
Njia hizo ni
pamoja na kutafuta wazalishaji wa mafuta wa nchi nyengine endapo wale wazalishaji wa awali watafunga
mipaka ya nchi zao katika kipindi hiko cha mpito.
No comments:
Post a Comment