Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, akimpa maelekezo mmoja ya wahandisi wanaotekeleza mradi mkubwa wa bomba la maji linatokea katika mitambo ya Ruvu Juu kuelekea katika maeneo mbalimbali ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo. (Picha na Voctor Masangu).
Mtendaji mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja
kulia akimpatia maelekezo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati
alipotembelea moja ya mradi wa maji ambao utawanufainisha wawekezaji wa viwanda
mbali mbali kikiwemo cha kuchakata nyama
katika eneo la Zegereni Wilayani Kibaha.
VICTOR MASANGU, PWANI
ZAIDI ya wakazi laki moja wanaoishi katika Halmashauri ya
Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambao walikuwa na kilio kikubwa cha
miaka mingi ya kukosa huduma ya maji safi na salama hatimaye wanatarajia
kuondokana na kero hiyo sugu ifikapo
Juni mwaka huu mara baada ya kukamilika
kwa mradi mkubwa kutoka eneo la ruvu juu hadi maeneo mbali mbali ya Chalinze ambao
umegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 16.
Hayo yalibainishwa na
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika ziara yake ya kikazi
yenye lengo la kukagua na kujionea miradi mbali mbali ya ujenzi wa maji katika
Wilaya ya Kibaha pamoja na mradi wa wami
ambao upo katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo na kuagiza mamlaka
husika kuhakikisha wanakamilisha mradi
huo kwa wakati ikiwemo sambamba na kufikishia huduma hiyo katika makazi ya
wananchi pamoja na maendeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda.
Aidha Ndikilo amezitaka taasisi zote nchini kuhakikisha
zinaachana na vitendo vya kuwa ni moja ya vigwazo katika kuwacheleweshea vibali mbali mbali wawekezaji
wa wa viwanda wa ndani na nje na badala
yake washirikiane nao bega kwa bega
katika kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025.
“Kwanza kabisa nimeamua kufanya ziara hii kwa lengo la
kuweza kujonenea miradi mbali mbali ya maji katika maeneo ya Mkoa wetu wa Pwani
na kwa upande wangu nimeweza kujionea jinsi ya mwenendo mzima, na kiukweli
nishukuru sana mtendaji mkuu wa Dawasa pamoja sa safu yake yote kwa kuweza
kufanya kazi ambayo inatia moyo ya kutekeleza kwa vitendo miradi ya usambazaji
wa maji katika maeneo ya viwandani pamoja na kwa wananchi wenyewe hii ni hatua
kubwa sana katika Mkoa wetu,”alisema Ndikilo.
Pia alibainisha kwamba kukamilika kwa miradi mbali mbali ya
maji katika Mkoa wa Pwani kutaweza kuwavutia wawekezaji wa viwanda kuwekeza
katika miradi mbali mbali sambamba na kuweza kutoa fursa za ajira kwa vijana
hivyo amewaomba wamiliki wa viwanda hivyo kuhakikisha wanawapa kipaumbele zaidi
wazawa katika suala zima la upatikanaji wa ajira lengo ikiwani ni kujiongezea
kipato na kuondokana na wimbi la umasikini.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian
Luhemeja baada ya kutembelea baadhi ya
miradi ambayo ipo kwenye mpango wa
kupatiwa maji ikiwemo viwanda amesema
kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba
wanatekeleza kwa vitendo azma ya kumuunga Mkono Rais wa awamu ya tano
katika kuwa na uchumi wa viwanda pamoja na kuwaondolea kero wananchi ambayo
wamekuwa wakiipata kwa kipindi kirefu kwa
kuwasambazia huduma ya maji safi na salama.
Mhandisi Luhemeja aliongeza kuwa latika jitihada za
kuboresha huduma ya maji katika maeneo
mbali mbali Dawasa iliingia mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba kuu la
kusafirisha maji lenye uumbaro wa kilometa 59 kutoka katika mitambo ya ruvu juu
hadi katika kijiji cha Mboga kilichopo katika halmashauri ya Chalinze na
utekelezaji wake unaendelea vizuri.
“Ujazo huu wa mradi mkubwa wa kutoka mlandizi hadi chalinze
unatarajiwa pindi utakapomalizika utasafirisha kiasi cha lita za ujazo milioni
tisa na laki tatu kwa siku moja ambazo zitaweza kuwahudumia wakazi wapatao laki
moja na ishirini sambamba na maunganisho mapya ya wateja zaidi ya elfu 18 ambao
wataweza kunufaika na mradi huo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Chailzinze Chalinze Rizone Kikwete alisema kwamba wananchi wake kwa kipindi cha miaka
mingi wamekuwa na adha kubwa ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama hivyo
kukamilika kwa mradi huo utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika maeneo mbali mbali ambayo yalikuwa
yanakabiliwa na changamoto sugu ya
kutembea umbari mrefu kwenda kutafuta maji katika maeneo mengine ya mbali.
“Hapo awali wananchi
wangu wa chalinze walikuwa wana kero kubwa sana ya kipindi kirefu kutokana na
ukosefu wa huduma ya maji, maana walikuwa wanatembea umbari mrefu kwa ajili ya
kwenda kutafuta maji lakini napenda kumshukuru sa Rais wetu Dk. John Pombe
Magufuli kwa kuweza kutoa kiasi hiki cha fedha ambacho kitasaidia kuleta neema
kwa wananchi hawa kwani kwa sasa wao wenyewe wanajionea jinsi ya utekelezaji wa
mradi huu na maswali yamepungua kabisa kila kona, alisema Rizone.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani yupo katika ziara yake ya kikazi ya
siku mbili katika baadhi ya Wilaya kwa lengo la kugagua na kujionea shughuli
mbali mbali zinazotekelezwa katika miradi
mbali mbali ya maji ambayo imelengwa kuwafikia wananchi pamoja na maeneo
ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na mambo mengine.
No comments:
Post a Comment