JARIDA
mashuhuri duniani la African Leadership limempa tuzo ya heshima katika
uongozi kwa mwaka 2019; Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela.
Utoaji
wa tuzo hiyo ya nane kwa viongozi wa Afrika waliofanya mambo makubwa
kwenye taasisi ama maeneo wanayoyaongoza ulifanyika hivi karibuni
jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Tuzo
hiyo iliasisiwa ili kutambua mchango wa kiongozi katika Bara la Afrika
ngazi ya wakurugenzi na namna anavyopenyeza biashara yake na kuwafikia
wengine kwa urahisi na kuaminika katika kujenga imani na ushindani wa
taasisi yake barani Afrika.
Akizungumzia
tuzo hiyo ya heshima, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Machi
4,2020; Nsekela alisema anafurahi na kuipokea heshma hiyo huku
akiwashukuru zaidi watanzania, wafanyakazi na wateja wa benki ya CRDB.
"Kwa
unyenyekevu nimeipokea tuzo hii ya heshima nikitambua kwamba ni matokeo
chanya ya juhudi, biashara na huduma zetu bora... ninawashukuru sana
African Leadership Magazine kwa kutambua na kuithamini kazi yetu,"
alisema Nsekela.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali mstaafu Gaudence Milanzi
aliyeshuhudia utoaji wa tuzo hiyo ya heshima, alipongeza juhudi za
Nsekela katika utendaji wake wa kuleta mabadiliko chanya kwenye Benki ya
CRDB na sekta ya fedha Tanzania na Afrika.
Akipokea
tuzo ya heshima kwa niaba ya Nsekela, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Benki ya CRDB, TulliEsther Mwambapa alisema hiyo ni ishara ya uongozi
imara wa benki yao na usimamizi madhubuti wa kanuni za msingi za
uendeshaji wa taasisi hiyo kongwe ya fedha hapa nchini.
"Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Nsekela pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa
Mabenki Tanzania (TBA) hiyo ni ishara kwamba utendaji wake kwenye sekta
ya fedha ni bora ndio maana amepata tuzo hii... anafanya juhudi kubwa
kuleta mabadiliko ya uendeshaji wa sekta hii ili iwe bora zaidi ndani na
nje ya Tanzania.
"Nsekela anasaidia kuijenga vema sekta ya fedha kwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa kukuza uchumi wa jamii," alisema Mwambapa.
Hafla
ya utoaji wa Tuzo ya Heshima ilibebwa na kaulimbiu isemayo 'Afrika kwa
Waafrika katika kuunganisha Bara lao' iliyohidhuriwa na wafanyabiashara
na viongozi wasimamizi wa sera za fedha kutoka nchi mbalimbali Afrika
akiwemo Naibu Rais wa Afrika Kusini, David Mabuza.
Viongozi wengine wa serikali waliokuwepo ni Deputy President, Republic of South Africaand Her Excellency, Nkosazana Dlamini-Zuma, Minister for Corporative Governance and Traditional Affairs, South Africa.
No comments:
Post a Comment