Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, amewaagiza wata alaamu wa Afya
Wilayani hapo kuanza mara moja kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona
kwenye nyumba za Ibada ikiwemo Makanisani na Misikitini.
Aidha Chongolo ameagiza pia elimu hiyo kutolewa kwenye vituo vya daladala ili
kuwasaidia wananchi kutambua namna ya kutumia na kujikinga na Virusi hivyo.
Chongolo ametoa agizo hilo leo katika kikao cha zarura kilichofanyika katika ukumbi
wa Afya ambapo kimehusisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Idara ya Afya,
watendaji pamoja na viongozi wa Dini .
Amesema kuwa
lengo la kikao hicho cha zarura ilikuwa ni kujadili namna na hatua zitakazo chukuliwa katika
kudhibiti virusi hivyo ili visiweze kusambaa pamoja na kutoa elimu ya kutosha
kwa watumishi sambamba wananchi katika Wilaya hiyo.
Amesema kutokana
na kuingia kwa Virusi hivyo vya Corona katika
jiji la Dar es Salaam, wataalamu hao wa Afya wa Wilaya hiyo wanapaswa kutoa
elimu madhubuti kwenye maeneo ambayo ni lazima wananchi kuyatumia kama vile
Vituo vya daladala ikiwemo vya mwendokasi, nyumba zaibada kuhusu namna ya
kujikinga na virusi hivyo.
Amefafanua
kuwa katika elimu hiyo pia itajikita katika kuelimisha wananchi namna ya
kutumia vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo kama vile vifaa vya kusafishia
mikono, Gloves na Barakoa (Mask) za kufunika pua na mdomo.
“ Hili jambo
tunapaswa kulichukulia kwa tahadhari kubwa, muwaelimishe wananchi kuhusu namna
ya kujikinga na Virusi hivyo, pamoja na kutumia hivyo vifaa ,mnapopita kwenye
hayo maeneo hakikisheni kwamba mnawaelimisha vizuri ili wajue ni wakati gani
wanapaswa kuvitumia, pia kusafisha miko mara kwa mara” amesema Chongolo.
“ Lakini pia
tuwasaidie wananchi kutoka kwenye presha waliyo kuwa nayo hivi sasa, tunafahamu
kuwa watanzania wengi wamepata taharuki juu ya Vizuri hivi, tusipojitahidi
tutajikuta tatizo la presha lina adhiri wananchi kuliko Vizuri vya Corona.
Katika hatua
nyingine Mhe. Chongolo amewaeleza viongozi wadini kwamba mikusanyiko isiyokuwa
ya lazima haipaswi kuwepo ila kwa ambao wanataka kufunga ndoa wafungishwe
lakini kwa kufuata utaratibu ambao utaepusha mikusanyiko ya watu.
Awali Kaimu
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, John Kijumbe amesema kuwa hadi sasa
wameshachukua tahadhari na kama vile kutoa
elimu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa watumishi na wahudumu wa Afya pamoja
na kugawa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.
Hata hivyo
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejidhatiti kikamilifu katika kujikinga
na virusi hivyo kwakuweka visafisha mikono kwenye mageti yote ya kuingia ikiwa
ni katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anayefika kupata huduma mbalimbali
wanakuwa salama.
Imeandaliwa
na Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment