HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 03, 2020

DStv yaja na ‘Jiongeze tukuongezee’

*Mteja akilipia kifurushi cha juu yake kuunganishwa cha juu zaidi bila gharama ya ziada

Wateja wa DStv wanaendelea kufurahia ofa kabambe zinazotolewa na MultiChoice na sasa imezindua kampeni mpya ya ‘Jiongeze Tukuongezee’ ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huunganishwa na kifurushi cha juu zaidi bila malipo ya ziada.

Kwa kampeni hii mpya iliyoanza rasmi tarehe 1 Machi 2020 na ambayo itaendelea hadi mwisho wa mwezi Aprili 2020, mteja wa kifurushi cha DStv Bomba Tsh 19,000, akilipia cha ju yake ambacho ni Family Tsh 29,000, moja kwa moja ataunganishwa kifurushi cha Compact – Tsh 44,000 bila malipo ya ziada. Hivyohivyo mteja wa kifurushi cha DStv Family akilipia Compact, atapandishwa kwenda Compact Plus Tsh 84,00 wakati yule wa Compact akilipia Compact Plus ataunganishwa kifurushi cha juu kabisa cha Premium cha Tsh129,000.

“Kampeni hii ya Jiongeze Tukuongezee inaenda sambamba na mkakati wetu wa kuhakikisha kuwa wateja wetu kote nchini wanapata maudhui bora na mengi kadiri iwezekanavy kwa gharama nafuu kabisa amesema Hilda Nakajumo – Mkuu wa Thamani kwa Wateja wakati wa uzinduzi rasmiwa kampeni hiyo uliofanika katika ofisi za MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Hilda amesema wanatambua kuwa kwa sasa wateja wana uzoefu na ufahamu wa maudhui bora na ya hali ya juu yanayopatikana kwenye vifurushi vya juu vya DStv, hivyo wameona ni vyema kuwapa wateja fursa ya kufurahia maudhui hayo kwa gharama nafuu

Wateja wote wa vifurushi vya DStv Bomba, Family, na Compact watanufaika na kampeni hiii pale tu watakapolipia kifurushi cha juu yaki na hapo DStv itawapadisha kwenye kifurushi cha juu zaini bila malipo ya ziada. Wateja wa kifurushi cha Compact Plus wataendelea kunufaika na chaneli za kifurushi cha juu cha Premium wakati wote wa kampeni hii.

Kwa ofa hii, mwezi Machi utakuwa mwezi maalum kwa kila mteja wa DStv. Kila mteja atakayejiongeza na kulipia kifurushi cha juu atapandishwa ngazi na hivyo kupata maudhui ya kifurushi cha juu zaidi. Hii itawafanya wateja wa DStv kushuhudia maudhui kabambe kama vile ligi kubwa za kandanda duniana, michezo kama ndondi, mieleka, tenis, mbia za magari, riadha bila kusahau sinema na tamthilia mbalimbali maarufu duniani pamoja na chaneli za habari, utafiti na elimu.

Wateja wa Compact watakaojiongeza na kulipia compact plus, watarushwa hadi Premium na hivyo kushuhudia chanel za M-Net ambako huko kuna sinema mpya kali na maarufu.

Kwa wale wapenzi wa magari ambao ni wateja wa Family, wakijiongeza kulipia Compact watapandishwa hadi Compact Plus ambako huko watashuhudia Salvage Hunters: Classic Cars kwenye channel ya Discovery (DStv Channel 121) pamoja na Makala za uchunguzi katika  CBS Justice (DStv Channel 170). Wateja wa Bomba watakaojiongeza na kulipia Family watarushwa hadi Compact na kufurahia maudhui kabambe ikiwemo michezo ya ligi maarufu ulimwenguni kama ligi kuu ya uingereza.

Kampeni hii ya Jiongeze tukuongeze itaendelea kwa muda wa miezi miwili hadi mwisho wa mwezi April 2020

Kwa maelezo Zaidi kuhusu ofa kabambe za DStv tembelea www.dstvafrica.co. ili kuweza kujihudumia kirahisi pakua app ya MyDStv  na kwa kupata burudani ya kutazama DStv popote ulipo pakua app ya DStv Now.
 ________________________________

No comments:

Post a Comment

Pages