HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 03, 2020

MOROGORO-DODOMA HAKUNA MAWASILIANO BAADA YA BARABARA KUKATIKA

 Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inautarifu Umma kuwa sehemu ya barabara eneo la Kiyegeya (Magubike) katika Wilaya ya Kilosa kwenye Barabara Kuu ya Morogoro – Dodoma imekatika na hakuna mawasiliano kati ya Mikoa hiyo kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Kufuatia hali hiyo, TANROADS inawaomba watumiaji wa barabara ya Morogoro – Dodoma kutumia viunganisho mbadala ikiwemo barabara ya Morogoro – Iringa – Dodoma na mikoa mingine ya kanda ya kati katika kipindi
hiki ambacho matengenezo katika eneo hilo yakiendelea. TANROADS inasikitika kwa usumbufu uliojitokeza wakati tunaendelea na huhudi za kurudisha mawasiliano katika barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages