HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 16, 2020

Diamond Platnumz apamba uzinduzi Pepsi Max

 Rashid Chenja- Meneja Mafunzo Na Uwezeshaji SBC Tanzania Ltd.
 Diamond Platnumz-Balozi Pepsi Tanzania.
Pepsi MAX.


Na Mwandishi Wetu

MFALME wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepamba uzinduzi wa kinywaji kipya kinachojulikana kama Pepsi Max.

Uzinduzi huo ulifanyika jana kwa njia ya tovuti (online), katika kuendeleza ile dhana ya kupunguza msongamano wa watu wakati huu wa janga la corona, ambapo Diamond ambaye Balozi wa Pepsi, alikuwa sambamba na Meneja Mafunzo na Uwezeshaji wa Kampuni ya SBC Tanzania, Rashid Chenja.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Chenja alisema kwa zaidi ya miaka 20, SBC imekuwa ikijivunia kufanya biashara kwa mafanikio makubwa katika soko la Tanzania.

“Na kwa miaka yote hiyo, tumeweza kuwapatia Watanzania nafasi ya kufurahia vinywaji vyetu mbalimbali kama Pepsi, Mirinda, 7Up, Mountain Dew, Evervess na H2OH. Kupitia aina mbalimbali za vinywaji vyetu, tumeweza kuchukua nafasi kubwa kwenye mioyo ya Watanzania na kuwa sehemu kubwa ya maisha yao ya kila siku,” alisema Chenja na kuongeza.

Na leo hii, tuko hapa na habari njema, tunazindua kinywaji kipya kinachoitwa Pepsi Max, ambacho ni muendelezo wa kinywaji pendwa cha Chapa ya Pepsi.

“Ni kinywaji kinachoendana na wale wote wanaofanya mambo yao kitofauti, wale wenye ujasiri wa kufanya vitu vyao kwa ubunifu na wale wote waletao maendeleo chanya kwa kuvumbua njia tofauti za kufanikisha mambo yao kila siku. Na ndio maana tumekuja na Kampeni inayosema ‘Ishi Mpaka Max’.

“Ishi Mpaka Max, ni kampeni inayolenga kusheherekea na kuwatambua wale wote wanaojaribu kupata kile kilicho bora zaidi kupitia juhudi zao binafsi, wale wanaotumia fursa kikamilifu, wale ambao wanaotumia ubunifu katika kuhakikisha wanaishi maisha kikamilifu, iwe katika sanaa, michezo, masomo, mavazi au nyanja yoyote yenye kuleta mafanikio chanya katika maisha yao,” alisema Chenja na kuongeza.

“Kwetu sisi, ni muhimu kuwapa wateja wetu, bidhaa inayofanana na wateja wetu, bidhaa yenye tabia na muonekano unaoshabihiana na vile wateja wetu wanavyopenda kuonekana, na ndio maana uzinduzi huu unaongozwa na Balozi wetu Diamond Platnumz. Kwetu sisi tunaamini Diamond Platnumz ndio maana halisi ya tunavyosema ‘Ishi Mpaka Max’. 

Kwa upande wake, Diamond alisema; “Pepsi Max ni Cola yenye ladha ya kipekee yaani Maximum Cola. Ni ladha yenye Bold Character na inaendana na wale wote wanaofanya mambo yao kitofauti kama mimi.

Mimi ninaishi Mpaka Max. Yani kama unavyoona bling bling, pamba kali, ngoma za ubunifu kama wote... Kwa kifupi ni kila ninachofanya nafanya kwa ujasiri, najiamini na naweka ‘Maximum Efforts,”.

Chenja akimalizia uzinduzi huo, alisema; “Katika kuhakikisha kila mteja wetu anapata kufurahia Pepsi Max, tumeileta katika Chupa ya plastiki ya ‘take away’, Pepsi Max inapatikana katika ujazo wa Mililita 600 (au BIGI), kwa Sh. 1,000 na chupa ya mililita 330 kwa Sh. 500  tu.

Jipatie Soda yako ya Pepsi Max leo na utuonyeshe ni jinsi gani wewe... ‘Una ISHI MPAKA MAX’.

Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe kwa kutusikiliza, nikutakie siku njema. ‘Stay Safe’, Ishi Mpaka Max,”.

No comments:

Post a Comment

Pages