Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Arusha Haniu Haniu akipokea vifaa vya kusaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa mkuu wa mkoa vilivyotolewa na kampuni ya Tanalec Ltd ya mkoa hapa leo Leo kwenye Ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Ahmed Mahmoud, Arusha
Tanelec imeanza kufanya utafiti wa mashine za kusaidia wagonjwa kupumulia kwa mashine katika kudhibiti ugonjwa wa Covid 19 na magonjwa mengine.
Akiongea Meneja msaidizi wa Tanalec Michael Mangowi kwenye hafla fupi ya makabidhiano kwa serikali mkoa wa Arusha ya vifaa vya kutakasa mikono ambazo ni sabuni 100 sanjari na ndoo 100 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Covid 19.
Alibainisha kuwa taasisi hiyo kupitia wafanyakazi wake imeendelea na utafiti wa kutengeneza mashine hizo pamoja na mashine nyengine ya kupita na kumwagiwa dawa ya kutakasa mwili mzima kwa lengo la kuendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa wa covid 19.
“Tumejipanga kuhakikisha tunaendelea na utafiti wa kuhakikisha tunapambana na ugonjwa wa Covid 19 kusaidia vitakasa mikono na mwili ili kuweza kuisaidia serikali yetu dhidi ya janga la ugonjwa wa covid 19”.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo alishukuru kwa msaada huo kwa kuwa ugonjwa huo hauchagui viongozi wala mtu yoyote.
Alisisistiza kuwa Mkoa wa Arusha umejidhatiti katika kuimarisha udhibiti wa wahamiaji haramu wanaoingia maeneo ya mipaka haswa mpaka wa Namanga uliopo Wilayani Longido pamoja na mpaka wa Ngorongoro uliopo wilayani Ngororongoro unaopakana na nchi jirani ya Kenya.
Alisisitiza kuwa kunabaadhi ya watu wameshakamatwa kuhusiana na kupita katika mipaka kwa njia za kinyemela na kuziomba taasisi ,mashirika na watu mbalimbali kujitokeza kwaajili ya kuchangia vitu mbalimbali ili kudhibiti ugonjwa huu wa Corona.
Naye mmoja kati ya wanufaika na msaada huo wa kujikinga na Corona ,Mwenyekiti wa Stendi Kuu ya Mabasi Maulid Rajabu alishukuru kwa msaada huo na kusisitiza kuwa hivi sasa wanajitahidi kutoa elimu juu ya ugonjwa huo sambamba na kuhakikisha kila basi linakuwa na ndoo pamoja na sabuni kwaajili ya kunawia mikono.
|
No comments:
Post a Comment