Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akipata maelezo
kutoka kwa viongozi wa JWTZ wakati walipofika kukagua mipaka ya eneo
hilo ikiwa ni kujionea na mwisho kutoa maamuzi ya mgogoro huo.
Sehemu ya makazi ya wananchi wa eneo la Loswira kata ya Moshono ambao mkuu wa mkoa wa Arusha alipita kukagua mipaka yao na JWTZ kikosi
Cha 977 KJ kwenye mgogoro uliodumu kwa muda mrefu.
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesitisha kwa muda kuendelea na
shughuli yeyote kwenye eneo la Losirwa kata ya Moshono hadi Serikali
itakapotoa maelekezo mengine ambapo amewaonya wenyeviti wa mitaa kuacha
kuchukuwa fedha na kutoa vibali vya ununuzi wa ardhi kwenye maeneo yenye migogoro.
Aidha amezitaka
halmashauri za wilaya kuacha kutoa vibali vya ujenzi kwa wananchi kwenye
maeneo yenye migogoro kwa kuwa inaleta mikanganyiko kwenye jamii na
kuleta ugumu wakati wa kuitatua.
Gambo
ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea eneo lenye mgogoro
baina ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi Cha 977 KJ na
wakazi wa eneo la Losirwa kata ya Moshono jijini Arusha uliodumu kwa
muda mrefu.
Akizungumza baada ya kukagua eneo hilo na kusikiliza pande zote ametoa maagizo
hayo na kueleza kuwa wananchi waendelee kuwa watulivu hadi Serikali
itakapotoa maelekezo mapya kufuatia mgogoro huo.
Alisema
kuwa wananchi wengi wanajielewa kama kuna mtu anaendelea na ujenzi
aachie hapo hapo hadi Serikali itakapotoa maelekezo mapya.
"Tunaunda
tume ya wataalamu kupitia upya na watatoa mapendekezo baada ya taarifa
ndipo tutatoa maamuzi lakini kwa Sasa shughuli zote nimezisitisha"
Alibainisha
kuwa wenyeviti na tarafa na vijiji wanaopitishia watu vibali vya
kununua ardhi watawachukulia hatua za kisheria kwani wao ndio chanzo cha
kuwaingiza wananchi kwenye migogoro.
Kwa upande wao wananchi wa eneo hilo Regina Elias na Poulo Mollel
wakizungumza wameitaka Serikali kuangalia suala hilo kwa kina na kufanya tathmini upya kwani wao wameishi muda mrefu eneo hilo na wanategemea
maeneo hayo kwa kujipatia riziki zao za kila siku.
Walisema
kuwa fedha walizopata kama fidia bado hazilingani na maeneo yao utakuta
mtu amelipwa kiasi kidogo na mwingine amelipwa eneo kama hilo kiasi
kikubwa kwa eneo lenye ukubwa kama huo na tathmini imekaa muda wa miaka
sita ndipo malipo yamekuja kulipwa bila maandishi yeyote hali inayoleta
mkanganyiko kisheria.
"Tunaiomba
Serikali yetu kwa kuwa sisi tunategemea kilimo na tumeishi muda mrefu
1960 jeshi limenikuta hapa huku jina langu likiwa halipo kwenye orodha
ya malipo naambiwa nikae kifamilia kwani kwenye familia kuna malipo ya
fidia kwenye eneo langu naomba mkuu wa mkoa tuangalie kwenye suala
hilo"alisema Martha John bibi mwenye miaka 86.
No comments:
Post a Comment