Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ametoa rai kwa Taasisi ya Uhandisi
na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) kuhakikisha wanawasaidia wajasiliamali
wadogo na wa kati kubuni mashine za kutengeneza sukari pamoja na
kuchakata katani ili kufungua fursa ya ajira na ongezeko la viwanda nchini.
Mhe.
Bashungwa aliyasema hayo mkoani Arusha alipokuwa akizindua mashine 14 za kisasa
zinazoendeshwa kwa mfumo wa kompyuta yaani CNC zikiwa na thamani ya shilingi milioni 600 zilizotolewa
kwa fedha za Maendeleo za Serikali na za ufadhili wa shirika la kimataifa la
UNIDO.
Akizungumza
na watumishi wa taasisi hiyo Mhe. Bashungwa aliwataka TEMDO kuongeza kasi ya
kubuni mtambo mdogo wa kuchakata miwa ili kupata sukari ili kuongeza uzalishaji
na upatikanaji wa wa bidhaa hiyo sokoni.
Aliongeza
kwa kusema wafanyabiashara wanapandisha bei ya bidhaa hususani sukari sokoni,
lakini endapo TEMDO itatengezeza mashine za kutengeneza sukari kwa
wajasiriamali wadogo itawasaidia
kujikwamua kiuchumi na kusaidia upatikanaji wa sukari nchini.
Aidha
amewataka pia kuongeza kasi ya kubuni mashine
ndogo ndogo za kuchakata zao la mkonge kwa kiwango cha upatikanaji wa
nyuzi ili kuwasaidia wajasiliamli wadogo kutengeneza nyuzi wao wenyewe ili
waweze kuziuza na kujiongezea kipato
badala ya hali ilivyo hivi sasa ambapo wakulima wanategemea wazalishaji wakubwa
kununua bidhaa hiyo kwa kiasi kikubwa ambapo mkulima amekuwa hanufaiki.
Sambamba na
hilo Mhe. Bashungwa alikabidhi barakoa zenye thamani ya Tsh.500,000
zilizotolewa na TEMDO kwa mkoa wa Arusha
ikiwa ni sehemu ya kuungana na Serikali kupambana na ugonjwa wa Korona kwa
watoa huduma ya afya.
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Prof. Fredrick Kahimba aliishukuru serikali kwa
kuwawezesha kupata mashine hizo ambazo zitawezesha kuunda mitambo na mashine
mbalimbali kwa urahisi zaidi kuliko awali.
Aliongeza
kuwa “taasisi ya TEMDO imeendeleza shughuli mbalimbali zinazochangia maendeleo
ya Viwanda Tanzania na kuwawezesha wakulima na wajasiliamali wadogo, wa kati na
wakubwa kujipatia teknologia ya kuogeza uzalishaji mali.
Pia
alimuomba Waziri Bashungwa kusaidia kuharakishwa uundwaji wa bodi mpya ya
Wakurugenzi ya taasisi kwa kuwa liyokuwepo imemaliza muda wake.
Kwa upande
wake bi Restuta Mrosso ambaye ni mnufaika wa utaalamu unaotolewa na TEMDO
aliishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia ujuzi
wajasiriamali kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuwasaidia kupata nembo
ya Ubora (TBS).
Waziri wa
Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa akiongea na uongozi na menejimenti ya
Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) kabla ya uzindua
mashine 14 za kisasa zinazoendeshwa kwa mfumo wa kompyuta yaani CNC zikiwa
na thamani ya shilingi milioni 600
zilizotolewa kwa fedha za Maendeleo za Serikali na za ufadhili wa shirika la
kimataifa la UNID.- Arusha, leo tarehe 25 Aprili 2020. (Picha na Eliud Rwechungura, Wizara ya
Viwanda na Biashara).
Waziri wa
Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa {katikati} akikata utepe wa kuzindua
mashine 14 za kisasa zinazoendeshwa kwa mfumo wa kompyuta yaani CNC zikiwa
na thamani ya shilingi milioni 600
zilizotolewa kwa fedha za Maendeleo za Serikali na za ufadhili wa shirika la
kimataifa la UNID {kulia} Mkurugenzi
Mkuu wa TEMDO, Prof. Fredrick Kahimba, {kushoto} Afisa biashara mka wa Arusha - Arusha, leo
tarehe 25 Aprili 2020.
Waziri wa
Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa {kulia} akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi
Mkuu wa TEMDO, Prof. Fredrick Kahimba, {kushoto} kutengeneza mashine ndogo
za kukamua miwa ili kutengeneza Sukari
ambayo itawasaidia wazalishaji wadogo na kati kuanza kuzalisha sukari itakayosaidia nchi kuwa na utoshelevu wa
mahitaji ndani ya sukari ili kufika malengo
mwaka 2024/25 kuzalisha sukari ya kutosheleza Watanzania pia na ziada
kuuzwa nje ya nchi. - Arusha, leo tarehe
25 Aprili 2020.
Waziri wa
Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa akikikagua mtambo wa kuchomea taka za
hospitali uliotengenezwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania
(TEMDO) - Arusha, leo tarehe 25 Aprili 2020.
Waziri wa
Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa akikagua bidhaa za wajasiriamali
wadogo zinazochakatwa na mashine zilizotengenezwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) - Arusha, leo tarehe 25 Aprili 2020.
Mashine
mpya za kisasa zinazoendeshwa kwa mfumo wa kompyuta yaani CNC zikiwa na thamani ya shilingi milioni 600 zilizotolewa
kwa fedha za Maendeleo za Serikali na za ufadhili wa shirika la kimataifa la
UNID.- Arusha, leo tarehe 25 Aprili 2020.
No comments:
Post a Comment