Waziri wa Madini, Doto Biteko amelitaka
Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kusimamia ipasavyo Viwanda vya Mfano vya Uchenjuaji
wa madini ya dhahabu vya Katente-Bukombe na Lwamgasa-Geita alivyovizindua leo APRIL
26 na kuvikabidhi rasmi kwa shirika la Stamico.
Ujenzi wa viwanda hivyo visivyotumia
kemikali hatari ya zebaki ulifanywa na kampuni ya Tan Discovery MineralConsaltancy Limited inayosimamiwa na Rogers Sezigwa iliyoanza ujenzi wa mradi mwezi
Disemba, 2016 ikianziaLwamgasanakufuatianaKatentenaItungi- Chunya.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi
wa viwanda hivyo vya Mfano,Waziri Biteko amesema, itakuwa aibu kubwa kwa Stamico
endapo Viwanda hivyo vitafia mikononi mwao kwani Serikali imetumia gharama kubwa
katika ujenzi wa viwanda hivyo.
“Afe Kipa, afe beki ni lazima viwanda
hivi vifanye kazi” Biteko alisisitiza.
Aidha,Waziri Biteko amewahakikishia
wananchi na wachimbaji wadogo wa madini nchini kuwa, serikali ya Rais John
Magufuli inawajali na itawahudumia kwa gharama nafuu hivyo wasisite kupeleka mawe
kiwandani hapo ili waweze kuchenjuliwa dhahabu kwa kutumia teknolojia mpya na ya
kisasa na hivyo kuepuka kutumia zebaki na kuachana na utumiaji wa matimba kwenye
mashapo.
Amesema matumizi ya matimba wakati
wa uchimbaji yanasababisha uharibifu wa mazingira wakati zebaki huathiri afya za
wachimbaji hivyo waitikie na kuvitumia viwanda hivyo kwa faida zao.
“Tumetengeneza viwanda hivi kuwavutia
ninyi fanyebiashara” Biteko alisisitiza.
Pamoja na hayo, Waziri Biteko alimtaka
Mwenyekiti wa Bodi ya Stamico kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi hii pasipo
kucheka na watu wasiotimiza wajibu wao kwenye viwanda hivyo.
Sambamba na hayo amewataka Bodi pamoja
na Stamico kuhakikisha wananchi wanaozunguka viwanda hivyo wananufaika na uwepo
wa viwanda katika maeneo yao kwa kupata ajira ndogo ndogo kwa kufanya hivyo kutainua
uchumi wao.
Akizungumzia faida zitokanazo na uwepo
wa viwanda hivyo vya mfano, Waziri Biteko alisema ni pamoja na utoaji wa mafunzo
na maarifa kuhusu sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali kwa wachimbaji
wadogo, kutolewa elimu ya mfumo wa kuthamini mashapo ya madini yaliyopo ilikufanya
uchimbaji wenye tija, kuchenjua dhahabu pamoja na kukodishwa vifaa vinavyotumika
katika shughuli za uchimbaji kwa gharama nafuu pamoja na kutolewa elimu juu ya uongezaji
thamani madini na upatikanaji wa masoko.
Akizungumzia mchakato wa ujenzi wa
viwanda hivi vya mfano, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal
amesema, ujenzi huo nimatokeo ya Utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009
iliyosisitiza zaidi juu ya uendelezaji wa sekta ya madini hususani wachimbaji wadogo.
Amesema katika kutimiza azma
hiyo, Serikali ilianzisha mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini
(SMMRP) uliokuwa na awamu mbili, ya kwanza ni kuanzia 2009 hadi 2014 na awamu ya
pili mwaka 2015 hadi 2018 ambapo awamuya pili ya mradi ndipo viwanda vitatu vya
mfano vya uchenjuaji wa dhahabu vya Katente- Bukombe, Lwamgasa- Geita na Itumbi
–Chunya vilipoanza kujengwa baada ya kufanyika kwa utafiti wa kijiolojia chini ya
ushirikiano baina ya uongozi wa mradi, Stamico, Taasisi ya Utafiti na Jiolojia
Tanzania (GST) na wachimbaji wadogo.
Akizungumzia gharama ya ujenzi wa
viwanda hivyo Ollal alisema mradi wa Katente umegharimu kiasi cha shilingi bilioni
1.7 na Lwamgasa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.3 wakati mradi wa Itumba
Uligharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7 na hivyo kufanya miradi yote kutekelezwa
kwa kiasi cha shilingi bilioni 4.7.
Ollal ameongeza kuwa, uwepo wa tekinolojia
hii kwa wachimbaji wadogo itakuwa na manufaa kama vile; kupunguza kwa kiasi kikubwa
ajali migodini kwa kutumia sementi katika kuimarisha kuta, kurahisisha utoaji wa
mbale mgodini(Haulage system) kupunguza athari za kimazingira kwa kutokata miti
hovyo na kurahisisha ufungaji wa migodi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara
y aMadini, Prof. Simon Msanjila amelitaka Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kuisaidia
jamii inayozunguka viwanda hivyo vya mfano kuondokana na changamoto ya maji kwa
kuchimba kisima kiwandani hapo na kuiruhusu jamii kunufaika na huduma hiyo.
Aidha, Prof. Msanjila amewataka Stamico
kutoa nafasi za ajira kwa wananchi kutokana na ukweli kwamba wao ndio walinzi wa
viwanda hivyo. “Nitashangaa sana kuona wafanyakazi wakawaida wanatoka km 200
kutoka hapa wakati kijiji kimezungukwa na vijana mahiri na wachapa kazi”
alisistiza Prof. Msanjila.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo,
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel ametoa wito kwa watendaji na wasimamizi wa
vituo hivyo kuwa wazalendo katika usimamizi wa Viwanda hivyo vya uchenjuaji wa dhahabu.
Sanjari na hilo, ameelezea mikakati
ya mkoa wake kuelekea maonesho ya Tekinolojia ya uchimbaji wa madini kwa mwaka huu
kuwa ni pamoja na mkoa wake kuandaa uwanja maalum kwa ajili ya maonesho hayo ambapo
tayari ujenzi wa jengo la ofisi mbalimbali ikiwepo ya wataalamu wa Sekta ya madini
umefanyika.
Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wataalamu
na timu nzima ya Ujenzi wa viwanda hivi kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo
ili kuachilia utaalamu wao kwa watanzania wengine wenye nia ya kujiendeleza kupitia
sekta ya Madini.
Waziri wa Madini, Doto Biteko, katikati akijiandaa kukata utepe hafla ya uzinduzi
wa viwanda hivyo vya Mfano.
Waziri wa Madini, Doto Biteko, akisaini kitabu
cha wageni mara baada ya kuwasili kilipojegwa kiwanda cha kuchenjua dhahabu
bila kutumia kemikali ya zebaki cha Katente wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho
uliofanyika tarehe 26 Aprili, 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon
Msanjila, akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa viwanda vya kuchenjua
dhahabu vya Katente na Lwamgasa uliofanyika Katente mkoani Geita tarehe 26
Aprili 2020.
Mtaalamu wa kuendesha mitambo ya uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia teknolojia ya Kisasa Gabriel Masanyiwa akitoa maelezo ya hatua zinazopitiwa mpaka kupata dhahabu. |
Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita mara
baada ya hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha
Katente na Lwamgasa Mkoani Geita. Kiwanda hicho kimekabidhiwa kwa Shirika la
Madini la Taifa (Stamico) ili kukisimamia na kukiendesha.
No comments:
Post a Comment