Ofisa
Usalama, Afya Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Asas Cosmas
Charles(kushoto) akimkabidhi mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya mkoa
wa Iringa, Alfred Mwakalebela mtambo wa kisasa wa kutakasa mwili kwa
ajili ya hospitali hiyo. (Picha na Denis Mlowe).
Na Denis Mlowe, Iringa
KAMPUNI
ya Asas imegawa msaada wa mtambo maalum wa kutakasa mwili na barakoa
zaidi ya 1200 kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na
hospitali za ya wilaya kwa ajili ya kujinga na kuenea kwa Virusi Vya
Corona.
Msaada
huo umekabidhiwa jana kwa mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Iringa, Alfred Mwakalebela na Afisa Usalama, Afya Mazingira na Ubora wa
Kampuni ya Asas Cosmas Charles kwa niaba ya mkurugenzi wa uzalishaji wa
kampuni hiyo, Ahmed Salim Abri sambamba na kutoa msaada wa ndoo maalum
za kunawa mikono 80.
Akizungumza
na wanahabari mara baada ya kukabidhi msaada huo, mwakilishi huyo,
Cosmas Charles amesema kampuni hiyo imeamua kuunga mkono juhudi za
serikali kupambana na ugonjwa wa corona ambao umekuwa tishio nchini na
duniani kwa ujumla.
Alisema
kuwa kampuni ya Asas mkoa wa Iringa imekuwa mstari wa mbele katika
kusaidia jamii hasa katika suala zima la kupambana kuenea kwa virusi vya
corona mkoani hapa na kuweza kutoa misaada mbalimbali kwa jamii.
Alisema
kuwa kama kampuni wameitikia maagizo ya serikali kuhusu kuzingatia
masuala ya usafi katika maeneo ya kazi kama sehemu ya kupambana na
tishio la maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona na kutoa misaada
mbalimbali kwa jamii wakiwemo madereva bodaboda, umoja wa daladala kwa
kuwapatia vifaa mbalimbali vya kujinga dhidi ya maambukizi ya corona.
Alisema
kuwa wametoa msaada huo ambao mtambo maalum wa kutakasa mwili mzima
ambao ni wa kwanza kwa hospitali za rufaa za nyanda za juu kusini na ya
pili nchini kuwana na mtambo huo hali ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa
jamii na wafanyakazi wa hospitali hiyo kujikinga dhidi ya maambukizi
hayo.
Aidha
aliongeza kuwa jamii inatakiwa kuwa na utamaduni wa kujiweka safi
katika mazingira wanayoishi na hali ya hii ya kunawa mikono kwa sabuni
inatakiwa kuwa utamaduni ambao unafanyika kila siku kuliko kusubiri
changamoto kama hizi za gonjwa la corona.
Cosmas
alisema kuwa kampuni ya Asas ni wadau wakubwa katika masuala ya afya na
wadau wa maendeleo kwa ujumla hivyo msaada huo ni kuhakikisha wananchi
wote wanaenda katika hospitali hiyo wanajikinga na maambukizi ya virusi
vya Corona ambavyo vimekuwa vinahatarisha maisha ya binadamu kote
duniani.
Kwa
upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa , Alfred Mwakalebela
alisema kuwa msaada umekuja wakati muafaka katika mapambano dhidi ya
kuenea kwa virusi vya Corona na kuwashukuru kampuni ya Asas kwa kuwa
mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya afya.
Alisema
kuwa kampuni hiyo imekuwa ikisaidia maeneo mbalimbali katika hospitali
hiyo ikiwemo ujenzi wa wodi ya watoto, nyumba ya damu salama, ujenzi wa
ICU ya kisasa pamoja na mashine zake ununuzi wa Xlay ya kisasa na bila
kuchoka wametoa mtambo bora kabisa wa kutakasa mwili mzima.
Alisema
kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kujenga karakana ya kutengeneza viungo
bandia vya miguu na mikono ambayo inatarajia kuanza kufanya kazi hivi
karibuni hali ambayo imesaidia kwa kiasi kubwa kuifanya sekta ya afya
kujivunia uwepo wake.
Mwakalebela
alisema kuwa kampuni hiyo imefanikiwa pia kuwapatia ndoo maalum za
kunawa mikono 80 ambazo watazitumia kuzigawa kwa vituo vya vya afya na
hospitali za wilaya na kuahidi kuvitumia vyema na kuwapa elimu zaidi
wananchi wanaokwenda kupata huduma hospitali.
“Kwa
kweli kampuni ya Asas imekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi mkoani
Iringa na kikubwa zaidi sekta ya afya kwani wameweza kuitendea haki kwa
kweli na kuwataka wadau wengine kujitoa kama ambavyo kampuni hiyo
imekuwa mstari wa mbele kujitoa kwa jamii.
No comments:
Post a Comment