Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelekezo ya Mkoa katika Baraza la Madiwani lilifanyika leo.
Na
Tiganya Vincent
HALMASHAURI
ya Mji wa Nzega hadi sasa imefanikiwa kutoa mikopo ya shilingi milioni 90 kwa
vikundi mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa jana
na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Philemon Magesa wakati wa kikao cha
Baraza la Madiwani.
Alisema
shilingi milioni 40 zimetolewa kwa vikundi 26 vya wanawake, shilingi milioni
33.6 wamekopeshwa vikundi 12 vya vijana na vikundi vinne vya watu wenye ulemavu
wamekopeshwa shilingi milioni 16.
Magesa alisema vikundi
vya wanawake na walemavu wamekuwa warejeshaji wazuri ukilinganisha na vikundi
vya vijana.
Alisema hadi hivi sasa
kwa kutumia Kitengo cha Sheria wanaendelea kuwafuatilia na kuwachukulia hatua
wadaiwa wanaosumbua ikiwemo kuwafiksha katika vyombo vya sheria.
Magesa aliongeza kuwa
katika kufuatilia madeni wamefanikiwa kurejesha shilingi milioni 17.7 ambapo
kati ya hizo milioni 5.3 zimerejeshwa na vikundi vya vijana , milioni 9.3
zimerejeshwa na wanawake na milioni 3.1 zimerejeshwa na vikundi vya watu wenye
ulemavu.
Kwa upande
wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ameipongeza Halmashauri ya Mji
wa Nzega kwa kuweza kutoa Mikopo ya
Vikundi vya Wanawake, Vijana na wenye Ulemavu kwa asilimia 100.
Aliutaka
uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanawafuatilia wadaiwa kwa ajili ya kurejesha fedha walizokopeshwa ili ziweze
kusaidia vikundi vingine.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya Mji wa Nzega hadi sasa imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 1.2 ambayo ni sawa na asilimia 61 ya lengo la
shilingi bilioni 2.
Alisema
hadi mwisho wa mwaka wa fedha huo wanatarajia kuviuka lengo la kitaifa.
No comments:
Post a Comment