Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, ameiagiza Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Rukwa kumchukulia hatua
za kinidhamu Afisa uhamiaji wa Wilaya ya Nkasi aliyechukua Rushwa ya Shilingi
315,000/= kutoka kwa wahamiaji wa nchi ya Burundi aliyekuwa anapita nchini
kuelekea nchi za kusini mwa Afrika.
Mh. Wangabo amesema
kuwa serikali haiwezi kukubali mtumishi mmoja kuvichafua vyombo vya ulinzi na
usalama na kuongeza kuwa mtumishi huyo anatakiwa kuwa fundisho kwa maafisa
wengine wa vyombo hivyo kwani wao ndio wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa aktika
kutii sheria na sio kinyume chake.
“Ni lazima achukuliwe
hatua kali sana huyu mtumishi na sielewi ni kwanini hajachukuliwa hatua hizo za
nidhamu mpaka sasa hivi, na iwe fundisho kwa mafias wengine kwenye vyombo vya
ulinzi na usalama, ni lazima waonyeshe mfano kwa watu engine lakini sio unakuwa
mfano wa kuchukua fedha chafu,” Alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu
wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Rukwa Hamza
Mwenda amesema kuwa fedha hizo zimerejeshwa na Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Nkasi
baada ya TAKUKURU kubaini kuwa mtumishi huyo alipokea kiasi hicho cha fedha
kutoka kwa wahamiaji wa nchi ya jirani.
“Wahamiaji hao
walikuwa wakisafiri kwa kwa basi kupitia nchini mwetu kwenda nchi za kusini mwa
Afrika wakiwa na vibali vyote na kueleza kuwa alipokea fedha hizo kama zawadi, pamoja
na kuchukuliwa hatua za kinidhamu, alitakiwa kurejesha fedha hiyo ambayo
itaingizwa kwenye akaunti maalum ya Benki kuu,” Alisema.
No comments:
Post a Comment