HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2020

CPB YAWAPIGA MSASA WAFANYAKAZI KINU CHA KUSAGA NAFAKA

 BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, (CPB), tawi la Arusha, Iddi Mkolomasa akiwanoa  wafanyakazi  wanapoendesha kinu cha kusaga na kukoboa cha Arusha.
 Meneja wa Udhibiti wa Viwango Kanda ya Kaskazini, (TBS), William Mhina akifungua mafunzo hayo.
 BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, (CPB), tawi la Arusha, Iddi Mkolomasa, akiwanoa  wafanyakazi wanapoendesha kinu cha kusaga na kukoboa cha  Arusha.



NA GRACE MACHA, ARUSHA

BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, (CPB), tawi la Arusha limeendelea kutekeleza mikakati yake ya kuhakikisha linaendelea kuteka soko la walaji ambapo limeanza kuwapatia mafunzo kwa wafanyakazi wake juu ya  namna bora ya uaandaaji na uchakataji wa nafaka ili kupata chakula bora na kisafi.


Mafunzo hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi zao ambapo yalifunguliwz rasmi na Meneja wa Udhibiti wa Viwango Kanda ya Kaskazini, (TBS), William Mhina


Kaimu meneja wa CPB tawi la Arusha, Iddi Mkolomasa aliwaambia wafanyakazi hao wanaoendesha kinu cha kusaga na kukoboa cha  Arusha kuwa wanapojipanga kuingia kwenye soko la kimataifa baada ya kukubalika kwenye soko la ndani hawana budi kuijua na kusimamia msingi ya kuandaa nafaka kwa kiwango cha kimataifa.



“Ni muhimu kuzingatia na kujua misingi na kanuni bora za uzalishaji chakula zikiwepo eneo la kuhifadhi, ukaushaji mzuri na kutengeneza kumbumbu za maandishi ya mfumo ili kuweza kujua chakula kitakachotumiwa na mlaji bila kuleta madhara,”alisema Mkolamasa.


Alisema kuandaa nafaka kwa ajili ya chakula bila kufuata mfumo wa kuandaa chakula ubora kunasababisha mlaji kupata madhara makubwa yakiwemo maradhi ya tumbo, kuharisha , kichefuchefu, kuumwa kichwa na maradhi mengine yanayotokana na maandalizi mabaya ya chakula.


Alisema mfumo mzima unasisitiza umuhimu wa kuandaa chakula ikiwepo usafi wa hali ya juu, kukausha ili kuondoa unyevunyevu ,kuhifadhi na kusafirisha katika mazingira yanayofanya chakula kumfikia mlaji bila kuleta madhara yoyote.

Akifungua afunzo hayo, meneja wa udhibiti wa viwango kanda,Mhina alisema kuwa mfunzo hayo ni muhimu haswa kwa wazalishaji wa chakula  kwa kuwa wafanyakazi wasipokuwa na elimu ya kuandaa chakula kwa ubora wanaweza kusababisha madhara makubwa kwa binadamu na viumbe wengine.

Alisema ni vema mafunzo kama hayo yakatolewa na wazalishaji mbalimbali wa vyakula jijini hapa jambo litakalosaidia kuwapunguzia shirika la udhibiti wa  viwango kazi ngumu wanayopata wakati wakifanya ukaguzi katika viwanda mbalimbali.

Mafunzo hayo yatakuwa yakifanywa mara kwa mara kiwandani hapo na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyo tawi la Arusha ambao ndiyo wanaendesha kinu cha kukoboa na kusaga nafaka cha (NMC).

No comments:

Post a Comment

Pages