Na Mwandishi Wetu
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la kwanza la udahili kwa mwaka wa masomo ya elimu ya juu 2024/2025 kuanzia leo July 15 hadi August 10 mwaka huu.
Akifungua Dirisha hilo Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU, Profesa Charles Kihampa Leo mbele ya vyombo vya habari amesema dirisha la kwanza la udahili kwa litakuwa wazi kuanzia leo July 15 hadi August 10 mwaka huu huku akitoa tafadhali kwa waombaji wote.
"Naomba taarifa hii ifike kwa wadau wetu wa elimu ya juu ndani na nje ya nchi na taarifa hii inahusiana na kufunguliwa rasmi kwa dirisha la udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa 2024/2025 kwa maana ya mwaka wa masomo.
"Kama nilivyosema dirisha hili litakuwa la kwanza, tunafungua dirisha la kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/25 na tunategemea kwamba dirisha hili litakuwa wazi kuanzia leo July 15 hadi August 10 mwaka huu.
"Utaratibu wa masomo ama utaratibu wa udahili kwa mwaka 2024/25 tuna makundi matatu ambayo tunatarajia ya wale ambao wataomba udahili."amesema Kihampa na kuongeza kuwa.
"Kundi la kwanza ni wale wenye sifa stahiki za kidato cha sita na hili ni kundi kubwa, lakini kundi la pili ni wale wenye sifa stahiki za stashahada kwa maana ya diploma ama sifa nyingine linganifu, sifa nyingine linganifu inawezeka kuwa ni mtu ana shahada lakini anataka kwenda kusoma shahada nyingine.
"Lakini kundi la tatu ni wale wenye sifa stahiki za cheti cha awali cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania inayojlikana kama 'Foundation Certificate' hili ndio kundi la tatu." Kihampa amebainisha kuwa.
"Kwa waombaji ili kufahamu sifa stahiki za makundi haya matatu ambayo nimeyataja wanashauriwa kwenda kusoma vitabu vya muongozo na vitabu hivi vya muongozo vinajulikana kama 'Bachelor Degree Admission Guide Box for 2024/2025 Academic Year', vitabu hivi vinapatikana katika tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu, ukiingia tu kwenye tovuti ya Vyuo Vikuu utaona pale vinaonekana vile vitabu, hapo sasa muombaji wa kundi lolote ataweza kujua na tuna vitabu viwili kwa wale wenye sifa stahiki za kidato cha sita na kingine ni kile chenye sifa stahiki kwa stashahada na sifa nyingine linganifu pamoja na cheti cha msingi.
"Utaratibu wa kutuma maombi ni kwamba maombi haya yanatumwa moja kwa moja kwenye Vyuo ambavyo muombaji amevichagua, kile Chuo anachokitaka ataingia kwenye tovuti ya Chuo hicho atakuta maelekezo mahususi ambayo yametolewa na Chuo. Kwaiyo muombaji anashauriwa zaidi ya kusoma ile miongozo kutoka kwenye tovuti ya Vyuo Vikuu aingie kwenye tovuti ya Chuo anachokihitaji atakuta maelekezo mahususi halafu atakuta namna ya kuweza kujisajili au kufungua akaunti yake ili aweze kutuma maombi yake ya kuomba udahili na vingezo na sifa za waombaji wa udahili."amesema.
Katika hatua nyingine amesema "Maswala muhimu ya kuzingatiwa na waombaji na ninaomba hili lieleweke vizuri, tumeweza kuweka kwa ujumla masuala makubwa manne ya kuzingatiwa. Jambo la kwanza ni kusoma kwa makini na kuelewa muongozo wa udahili ambao umetolewa na TCU lakini pia na maelekezo mahususi ambayo yametolewa na Vyuo kabla ya kutuma maombi.
"Lakini pia waombaji wanashauriwa kuingia katika tovuti za vyuo na kuwasiliana na vyuo moja kwa moja ili kujua taratibu za kutuma maombi na kupata taarifa taarifa za kina kuhusu programu za masomo ili kujiridhisha kabla ya kutuma maombi.
"La tatu ni kutuma maombi moja kwa moja vyuoni kupitia mifumo ya kimtandao, kwaiyo hakuna utaratibu wa kusema unampa mtu fulani zile taarifa zako au kuna fomu ambazo utajaza kwa maana ya nakala ngumu lakini muombaji anaingia kwenye Chuo husika atakuta mfumo wa kimtandao atajisajili pale halafu ataendelea kutuma maombi.
"Jambo la nne ni kwa wale waombaji ambao wana vyeti vilivyotolewa na mabaraza ya mtihani ya nje ya nchi hawa wanapaswa kuwasilisha vyeti vyao katika Baraza2 la mitihani la Tanzania kwa wale ambao wana vyeti vya Elimu ya sekondari."
Kihampa hakuishia hapo amesema "Lakini wale ambao wana vyeti vya stashahada hawa wanashauriwa kutuma kwanza vile vyeti vyao katika Baraza la ufundi na mafunzo stadi Nacte, watapeleka kule halafu wataweza kupata ulinganifu lakini pia wataweza kupata namba ambayo itatumika katika wao kutuma maombi yao vyuoni, namba hii inajulikana kama 'Award Verification'.
"Tume inapenda kuwahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU, tovuti za Vyuo vilivyoruhusiwa kudahili wanafunzi wa shahada ya kwanza pamoja na taarifa mbalimbali zinazotolewa na TCU kupitia vyombo vya habari kama ambavyo tunazungumza hapa Leo.
Aidha amehitimisha kwa kutoa tahadhali "Nitoe pia tahadhali kunapokuwa na jambo kubwa kama hili kunaweza kukajitokeza watu ambao wanakuwa kama wanakaa katikati, kwaiyo niwaombe kwamba waombaji wote wanaotaka kujiunga na shahada ya kwanza katika Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, maombi yanawasilishwa moja kwa moja kwenye Vyuo husika.
No comments:
Post a Comment