HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 29, 2020

KILIO CHA MUDA MREFU KWA WANA KAGERA CHAMALIZIKA

New Mv Victoria Hapa Kazi Tu 


Na Lydia Lugakila Kagera

Hatimaye meli ya New Mv Victoria Hapa Kazi Tu iliyokuwa imesitisha huduma za usafiri katika ziwa victoria kati ya
Mwanza na Kagera  imetia nanga katika bandari ya
Bukoba ikitumia muda wa takribani saa sita tofauti na saa
12 za awali.
 
 Meli hiyo iliyokuwa ikijulikana kama MV Victoria
imepokelewa   katika bandari ya Bukoba majira ya saa 10
jioni june 28 mwaka huu.
 
imeelezwa kuwa meli hiyo imeanza safari zake katika
bandari ya Mwanza majira ya saa 3 asubuhi na kwamba
ilisitisha huduma  kati ya mwanza na Bukoba  takribani
miaka sita iliyopita.
 
Mgeni rasmi katika hafra hiyo ya upokeaji wa meli hiyo
alikuwa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha
Mapinduzi (CCM)  Humphrey Polepole, ambaye alisafiri
na meli hiyo kutoka Mwanza hadi Bukoba na emeeleza
ujio wa meli hiyo ilivyo kielelezo tosha cha utekelezaji wa
ahadi ya CCM na maono ya Rais John Pombe Magufuli
kwa maendeleo ya watanzania,.
 

Pole pole amesema ameagizwa na Rais Magufuli
kuwatangazia wakazi wa kanda ya ziwa kuwa gharama za
kusafilisha mizigo zitakuwa ndogo kulinganisha na hapo
awali ambapo tani moja itasafirishwa kwa sh elfu 27 tofauti
na ilivyokuwa awali ya sh 120,000 kwa mzigo wa tani moja
 
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera Bregidia
General Marco Gaguti amesema  kuwa ujio wa meli hiyo
utafunguia fursa za kibiashara baina ya Kagera na mikoa
jirani pamoja na nchi zinazozunguka mkoa wa kagera
 
Ukarabati wa meli hiyo umegharimu zaidi ya Sh. Bilioni 22
na itakuwa na uwezo wa kubeba abiria na mizigo yenye
tani 100 na gharama za usafiri kati ya mwanza na Bukoba
pamoja na tarehe ya kuanza rasmi safari itatangazwa
baada ya siku 14 kuanzia sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages