Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd akisalimiana na Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Manispaa ya Shinyanga wakati wa ziara yake katika
Manispaa hiyo kuzindua jengo la Katibu wa Umoja wa Vijana CCM Manispaa ya
Shinyanga.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd mara baada ya kukata
utepe kuzindua jengo la Katibu wa Umoja
wa Vijana CCM Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga wakati ziara ya Makamu wa pili wa Rais wa
Zanzibar Barozi Seif Ali Idd iliyowakutanisha viongozi wa chama hicho Mkoani
Shinyanga.
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
Makamu wa pili wa
Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd ametaja sifa za Mgombea anayefaa kuwa Rais
wa Zanziba kuwa mtu ambaye ni mwamini mkubwa wa Muungano kwasababu kiongozi wa
sifa iyo kamwe hawezi kuleta mgawanyiko miongoni mwa watu wa Tanzania.
Barozi Seif Ali Idd
amesema hayo jana alipokutana na viongozi na wanachama wa CCM wa Manispaa ya
Shinyanga katika ziara yake kichama mkoani shinyanga inayoendelea baada ya
kufanya ziara kama hiyo katika Wilaya ya Kahama.
Barozi Seif aliongeza
kuwa kiongozi anayetaka kuwa Rais wa Zanzibar lazima awe yule asiyeweza
kutugawa na anayefuata misingi ya Muungano wetu akiongeza kuwa kwasasa kuna
watu wengi sana kutoka bara wanaofanya kazi zao Zanzibar na kuna watu wengi
sana kutoka Zanzibar wanaofanya kazi zao Tanzania bara.
Kiongozi huyo mkubwa
wa Serikali ya Zanzibar amesema mpaka sasa kuna idadi kubwa ya watu ambao
tayari wamechukua fomu za kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar ambao kimsingi
wanatimiza haki yao ya kidemokrasia na mchakato wa kumpata mgombea utajulikana
baada ya taratibu kukamilika.
Katika ziara yake
Mkoani Shinyanga Barozi Seif Ali Idd alianza na uwekaji jiwe la msingi katika
ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa Ummoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na
kuwataka vijana wa Chama Cha Mapinduzi kutoshiriki katika vitendo vya rushwa
hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Aidha amewaonya
vijana hao kutokubali kutumiwa kwasababu wagombea wengi upenda kuwatumia vijana
kufanikisha malengo yao ya kisiasa na kuwataka kutumia wingi wao kufanikisha
uchaguazi hapa Nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Bi. Zainab Telack amewataka wagombea nafasi za ubunge Mkoani
Shinyanga kutotegemea Msaada wa aina yoyote kutoka Serikalini nakuwataka
wagombea hao kujipanga kulingana na matakwa ya chama na kuongeza kuwa serikali
itashirikiana nao baada ya kuwa mgombea kuwa amefanikiwa kupita katika mchakato
nakufanikiwa kuwa mgombea.
Bi. Telack aliongeza
kuwa kutakuwapo na watu wengi watakaojitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge
hivyo wagombea wote hao watambue kuwe hawana nafasi yoyote ya kupata msaada
kutoka ofisi yake bali wazingatie taratibu zilizowekwa na chama kukidhi matakwa
ya taratibu za uchaguzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
yuko Mkoani Shinyanga kwa ziara ya Kichama na ataendelea ziara yake katika
Wilaya ya Kishapu na kuendelea kufanya shughuli za Chama kwa kuwa ni mlezi wa
Chama hicho Mkoani Shinyanga.
No comments:
Post a Comment