HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 29, 2020

NAIBU WAZIRI NYONGO AANZA ZIARA TUNDURU

Leo tarehe 29 Juni, 2020 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameanza ziara yake katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma yenye lengo la kukagua shughuli za madini, soko la madini, kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali. Amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro Mtatiro.

Akizungumza wakati wa ukaribisho Mtatiro ameleeza kuwa ofisi yake imekuwa ikishirikiana kwa karibu zaidi na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Ruvuma katika kutatua changamoto mbalimbali kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na soko la madini.

No comments:

Post a Comment

Pages