HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 23, 2020

Kongamano la michezo kufanyika Jumamosi

Na Mwandishi Wetu
 
KONGAMANO kubwa la michezo litafanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambalo litajadili athari za janga la virusi vya corona katika michezo nchini.

Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa kongamano hilo litashirikisha viongozi wa michezo wa mashirikisho, ambayo yako katika mfumo wa Olimpiki pamoja na waandishi wa habari za michezo nchini.

Tandau alisema kuwa walitaka kualika watu wengi, lakini wamealika 60 ili kuhakikisha wanazingatia umbali wa meta moja kati ya mtu na mtu wakati wa kongamano hilo muhimu.

Alisema kuwa awali walitakiwa kuwa na Siku ya Olimpiki, ambayo ilipangwa kufanyika Juni 21, lakini kutokana na corona hawakufanya na badala yake wataendesha kongamano hilo, ambalo litakuwa na manufaa kwa michezo nchini.

Akielezea mada zitakazotolewa siku hiyo, Tandau alisema ni pamoja na athari za virusi vya corona kwa michezo nchini, hasa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya 2020.

Nyingine ni changamoto na fikra za mipango ya michezo baada ya janga la ugonjwa wa Covid-19, pamoja na mchango wa michezo kwa muhimili wa maendeleo, Michezo ya Olimpiki ya 2020 ilipangwa kufanyika Tokyo, Japan kuanzia Julai mwaka huu kabla ya kuahirishwa kwa mwaka mmoja, na sasa itafanyika Julai 23 hadi Agosti 8, 2021.

No comments:

Post a Comment

Pages