Mchungaji Yohaness Chawinga wa Kanisa la GCIM Manzese Ubungo jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MUUNGANO wa vyama vya upinzani nchini Malawi wa Tonse Alliance chini ya mgombea Urais Dk. Lazarus Chakwera na mgombea mwenza Salous Chilima toka chama cha UTM wametabiriwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa marudio unaofanyika kesho.
Utabiri huo umetolewa na Mchungaji Yohaness Chawinga wa Kanisa la Huduma GCIM Manzese Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Chawinga alisema amekuwa akioteshwa kila mara kuhusu uchaguzi na Bwana Yesu baada ya Mahakama ya Kikatiba nchini humo kuufuta ushindi wa Profesa Athur Mutharika,uliofanyika mwaka Jana.
"Nimekuwa kwenye maombi yakuiombea Malawi tangu February mwaka huu mara nilipopata habari kupitia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ya kufutwa kwa matokeo ya uraisi yaliyompa ushindiMutharika.
Toka nilipoanza kuomba na kufunga Mungu amenipa jumbe kuhusu Malawi. Mosi mnamo Machi 15 kupitia ndoto Mungu alinichukua mpaka kazini kwangu nikiwa pale kazini jengo jipya nikamuona Dk. Lazarus Chakwera baada ya kukutana naye tukawa tunatembea kwenda jengo jipya la ofisini kwetu huku tukisukuma 'stretcher' na tukiongea lugha ya kimalawi kama Chitumbuka mara nikamwambia kwa kiswahili kuwa utakuwa raisi wa Malawi," alisema.
'Hii nikusema kuwa Mungu wa Mbingu na Nchi amempa kibali Mch Chakwera kuwa raisi wa Malawi. Hivyo huyo ndiye raisi ajaye wa Malawi.
Njia hii ya ujumbe kama huu wa kukutanishwa na mgombea wa uraisi kumwambia maneno kama haya imetokea kwa Rais Donald Trump na Rais Muhammadu Buhari. Mungu husema nasi kwa njia ya ndoto, Daniel 7:1 -2 Mwanzo 15:1 Mathayo 1:20,"alisema.
Alisema pili mwezi May alioneshwa amekutana na mwanamume mmoja wa Malawi ambapo alikuwa ameshika nguo nyekundu akampa yule mwanamume. "Hii naweza kusema kuna kumwagika damu nchini Malawi. Dalili ya jambo hili imeanza kutokea kwenye kampeni za mgombea mwenza wa Mch Chakwera Mheshimiwa Chilima watu wamejeruhi Kwa risasi na kupigwa mawe," alisema.
Mchungaji Chawinga alisema anawasihi wananchi wa Malawi na jamii ya waaminio kule Malawi na kwingineko kuombea uchaguzi uwe wa amani na haki.
No comments:
Post a Comment