HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 29, 2020

MWANAMUZIKI VITALI MAEMBE AJIUNGA NA ACT WAZALENDO

NA JANETH JOVIN

MWANAMUZIKI  wa nyimbo za ukombozi Vitali Maembe amejiunga na Chama cha ACT Wazalendo na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu katika Ofisi ya Chama Magomeni.

Akimkabidhi kadi ya uanachama, Shaibu  amemhakikishia Maembe kuwa ACT Wazalendo litakuwa jukwaa sahihi kwake kuendeleza mapambano ya kudai haki, kupinga rushwa na kupigania umoja wa Afrika kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote kupitia sanaa.

Maembe aliyewahi kuimba nyimbo ya "Sumu ya  teja", "vuma" nk alitumia fursa hiyo pia kutangaza nia ya kugombea Ubunge kwenye Jimbo la Bagamoyo.
Mwanamuziki wa nyimbo za ukombozi Vitalu Maembe akikabidhiwa kadi ya Chama cha ACT Wazalendo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu.

No comments:

Post a Comment

Pages