Anaandika Malisa GJ
Saniniu
Laizer mchimbaji mdogo wa madini huko Mererani ameamka Bilionea baada
ya kupata mawe mawili ya Tanzanite moja lenye uzito wa 9.2KGs na jingine
5.8KGs yenye thamani ya TZS 7.8 Bilioni.
Watu
wengi wanajadili kuhusu Tanzania kumpata Bilionea mpya. Ni jambo zuri
lakini kuna jambo jingine ambalo halijadiliwi. Na pengine ni la msingi
zaidi kuliko Ubilionea wa Laizer.
Hii
Tanzanite ya 9.3KGs inaweza kuwa ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana
duniani. Hii ndio "angle"ya habari, ambayo inaweza ikabreak (as breaking
news) ikatoa day 2 story na ikatengenezewa developing story hata kwa
mwezi mzima.
Kabla ya
Laizer kuushangaza ulimwengu kwa kuchimbua ardhi na kupata madini haya
makubwa kabisa, Tanzanite kubwa zaidi duniani ilikua na uzito wa 3.3KGs
na 16,839 carat. Hii ilichimbwa na kampuni ya TanzaniteOne mwaka 2005.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.mining.com
Tanzanite hiyo yenye uzito wa 3.3KGs ipo Thailand katika mji wa
Bangkok. Wathai wameamua kuifanya fursa ya utalii. Wanatangazia dunia
kwamba "karibu Thailand uone Tanzanite kubwa zaidi". Na watu wanasafiri
kila pembe ya dunia kwenda kuona hicho kinachoitwa Tanzanite kubwa zaidi
na kupiga nayo picha. Utalii wa aina yake.
Kwa
kufanya hivyo Thailand iliweza kurudisha fedha ilizotumia kununua
Tanzanite hiyo ndani ya miaka minne tu. Na kuanzia 2010 wanapata faida
(super normal profit). Mradi huo umeiingizia Thailand pesa nyingi sana
na kutoa ajira kwa watu wengi.
Sasa
ni wakati wa kibao kugeuka. Na sisi tutengeneze kituo tuweke haya mawe
ya Laizer na tuiambie dunia kuwa Tanzanite kubwa zaidi ipo Tanzania na
si Thailand tena. Watu waje washangae hayo mawe wapige nayo picha
watulipe 'dollars" wakamalizie picknick Serengeti. Wakitaka kumuona na
mchimbaji ruksa.
Hii
itatulipa zaidi kuliko kuyauza haya mawe kama tulivyofanya 2005. Pia
itafungua fursa mpya ya utalii wa madini ambayo hatujawahi kuwa nayo.
Tuige kwa Wathai lakini tufanye kwa ubora kuliko wao (ujasusi wa
kiuchumi).
_
Kama watu
waliweza kusafiri kutoka Marekani, China, UK etc kwenda kushangaa
Tanzanite ya 3KGs kule Bangkok, sisi tukisema tunayo ya 9KGs hata
shetani si anaweza kuja kushangaa kidogo akapate cha kusimulia kuzimu?
No comments:
Post a Comment