Balozi Seif Ali Karume akipokea Fomu kutoka kwa Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar na Idara ya Organization.
Kada wa CCM Balozi Ali Karume akionyesha mkoba uliokuwa na fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu
Makada wa wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Ali Karume
na Mbwana Bakari Juma wamefunguwa dimba la uchukuwaji wa fomu ya kuomba ridhaa kupitia chama hicho kugombea
nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Zoezi hilo la uchukuaji fomu limefanyika katika
Ofisi kuu za chama hicho Kisiwandui Mjini Unguja na kukabidhiwa na Katibu wa
kamati maalumu ya Zanzibar na idara
Organization Cassin Galos Nyimbo.
Balozi Ali Abeid Karume
ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar katika Serikali ya
awamu ya Saba ambaye pia ni mtoto wa muasisi Taifa Hili hayati Abeid Karume
Rais wa kwanza Visiwani.
Asubuhi mapema Mbwana
Bakari Juma alifika ofisini hapo kabla ya Balozi Ali karume aliyefika saa saba
mchana kufanya tendo kama hilo.
Juma ambaye ni mhandisi alikiomba chama hicho kumuamini kuwa
yeye anaweza kukiwakilisha chama hicho kwenye kuwania nafasi hiyo.
Mara baada ya kuchukua
Fomu Balozi Ali Abeid karume alisema kamba iwapo chama cha Mapinduzi
CCM kitampa ridhaa ya kuwa mgombea wa nafasi hiyo na kuwa Rais wa Zanzibar,
anatarajia kuendelea dhamira ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyalinda, kulinda Muungano
wa Tanganiyika na Zanzibar na kuendeleza Sera za CCM.
“Iwapo nitateuliwa na
chama changu na kupata ridhaa ya wananchi wenzangu, nategemea kuendeleza
dhamira ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kwa kuyalinda, kulinda Muungano na
kuendeleza Sera za CCM” Alisema Balozi Ali Abeid Karume.
Katika Maelezo yake
Balozi Ali Abeid Karume alisema kwamba Dk. Ali Mohamed Shein kwa kushirkiana na
Baraza la Mapinduzi amefanya kazi kubwa nay a kupigiw mfano katika kuendeleza
Sera zilizoainishwa na Mzee Abeid Amani Karume.
“Nia yangu ni
kuyaendeleza yale yote mazuri ambayo tumeachiwa na ambayo Jemedari wa
Mapinduzi yetu kama vile afya bure,Elimu bure, ugawaji wa Ardhi kwa wananchi na
ujenzi wa makazi bora kwa wananchi,”alisema Balozi Ali Abeid Karume.
Aidha Balozi ali abeid
Karume alisema ipo haja ya kuleta usawa wa Kijinisia, kuwalinda watoto,
kuwatunza wazee na kuwwapa vijana Elimu ya kujitegemea.
“Pia pindipo nitakuwa
mgombea nitakae chaguliwa na chama change na kupewa ridhaa na wananchi wa Zanzibar,
Ipo haja ya kuendeleza ujamaa, udugu, upendo na mshikamano ambapo vyete hivyo
ndio ngo zetu” alieleza Balozi Ali Karume.
Balozi ali Karume
aliwaomba Wananchi wa Zanzibar na Makada wa chama cha Mapinduzi CCM, kumuombea
kwa mwenyezimungu katika mchakato huo aliouanza pamoja na kuiombea Nchi na
jamii kuwa katika hali ya Amani na utulivu.
Hii ni mara ya Pili kwa
Balozi Ali Abeid Karume kuchukua fomu ya kugombania nafasi ya Urais wa Zanzibar
ambapo awali alichukua mwaka 2010 ambapo Dk Ali Mohamed Shein ndie alipitishw
na Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea na kushinda kuwa Rais wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment