HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 15, 2020

KAMANDA MUSLIM AWAKUMBUSHA POLISI KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA COVID 19 MKOANI SINGIDA


 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Fortunatus Muslim, akizungumza na madereva wa malori eneo la Mizani Mjini hapa wakati wa ziara yake ya siku moja ya kikazi.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Fortunatus Muslim, akizungumza na Askari wa Usalama Barabarani Mkoa wa Singida katika eneo la Mizani.
 Mazungumzo na askari hao yakiendelea.
 Kamanda Muslim akisisitiza jambo.
Kamanda Muslim akizungumza na madereva.


Na Dotto Mwaibale, Singida

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Fortunatus Muslim ametoa elimu ya kuchukua tahadhari  dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 kwa watendaji wa jeshi hilo, madereva na abiria mkoani Singida.

Akizunguza na waandishi wa habari mjini hapa jana alisema amefika kwa ziara ya siku moja ya  kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida wa barabarani na kuangalia hali ya utendaji wa askari wa jeshi hilo na mwenendo wa vyombo vya moto.

Alisema nia kubwa ni kutoa elimu na kuhakikisha kwamba wanathibiti ajali za barabarani na kukumbushana kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona.

" Leo nimeanza kufanya kazi eneo la Mizani  pale Njuki kwa kuzungumza na madereva wa malori kuhusiana na mwendo kwamba bado ni tatizo na kuwa ni chanzo kikubwa cha ajali zinazotokea  barabarani nimetoa mfano wa ajali iliyotokea mkoani Mwanza ambapo lori lilikwenda kugonga trekta ambalo lilipoteza mwelekeo na kwenda kugonga gari la abiria na kusababisha vifo vya watu nane huku watano wakijeruhiwa" alisema Kamanda Muslim.

Alisema alikuwa anajaribu kuonesha madhara yanayosababishwa na mwendo kasi kwamba tumepoteza watanzania ambao tulikuwa bado tunawahitaji kwa kufanya kazi ili kuweza kuinua uchumi na kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Muslim alisema pia ametoa elimu kwa madereva kuhusu matumizi ya tochi wanazozitumia kukamata mwendo wengi wamekuwa wakilalamika kwamba picha zinazopigwa na kutumwa kwenye simu zinachezewa wakati sio kweli hivyo nimewaonesha namna gani tochi hizo zinavyounganishwa kwenye simu na  kwamba  muungano huo unafanyika ndani kwa ndani ya ile kamera na askari hawezi kuifanyia mabadiliko yoyote.

Alisema hivi sasa wapo kwenye utaratibu wa kuanza kutumia kifaa kipya ambacho watakitumia kupokea hizo picha kwa nchi nzima hivyo amewasihi wazingatie sheria, alama na michoro ya barabarani badala ya kuendesha huku wakitafuta askari yupo wapi.

Muslim alisema amewaambia madereva hao kuyaondoa magari yao barabarani pale yanapokuwa yameharibika kwa kuyatengeneza haraka na waache tabia ya kuweka majani na miti kwani inapofika usiku magari mengine yakijaribu kuyapita wanashindwa kuyaona hivyo kujikuta wakiyagonga na kusababisha ajali.

Akitolea mfano alisema juzi waliyakamata mabasi mawili yaliyokuwa yakipishana mlima Saranda ambapo alizungumza na madereva wa malori kuwa kuanzia sasa hawatasimamishwa katika sehemu nyingine yoyote isipokuwa kwenye maeneo ya mizani.

Alisema sehemu nyingine wanazoweza kusimamishwa ni iwapo kutakuwa na taarifa za kiinterejesia kwamba yamebeba vitu kinyume cha sheria au yamesababisha ajali au yamefanya makosa barabarani au kama madereva hao leseni zao zinadaiwa faini za makosa ya usalama barabarani hivyo amewataka walipe ili kuepuka kusimamishwa hovyo barabarani kwa ajili ya hayo madeni.


Alisema akiwa Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Singida amezungumza na madereva na kuwasisitizia kuacha kwenda mwendo wa kasi kwani Serikali yetu ni sikivu imeruhusu kusafiri usiku hivyo hakuna sababu ya kwenda kwa mwendo wa kasi.

No comments:

Post a Comment

Pages