Na Janeth Jovin
BENKI
ya Standard Chartered Tanzania imetoa msaada wa Sh. Bilioni 1.2 ambazo
ni sawa na dola za kimarekani 550,000 kwa Chama cha Msalaba Mwekundu
Tanzania (Red Cross) na kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Watoto (UNICEF).
Katika
taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam
ilieleza kuwa kati ya fedha hizo, Sh. Milioni 690 ambazo ni sawa na dola
za kimarekani 300,000 zimekabithiwa kwa Red Cross Tanzania kwa ajili ya
kuwezesha upatikanaji wa dhana za kujikinga ikiwepo maji safi na salama
na sabuni.
Ilieleza
kiwa kiasi cha Sh.Milioni 575 sawa na dola za kimarekani 250,000,
zimekabidhiwa kwa UNICEF kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu hususan kwa
watoto waishio katika mazingira yenye changamoto.
"Misaada
hii ni sehemu ya ahadi ya Standard Chartered PLC ya dola milioni10
ambapo milioni tano kwa msalaba Mwekundu na dola milioni 1.5 kwa UNICEF
ambazo zitawasaidia katika shughuli za dharura hasa wakati huu wa
mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 huko Asia na Afrika," ilieleza taarifa
Aidha
ilieleza kuwa Sanjay Rughani ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
hiyo ya Standard Chartered Tanzania, alisema "Standard Chartered
Tanzania inajivunia kuweza kuchangia juhudi mbalimbali za Msalaba
Mwekundu na UNICEF zinazowafikia watu walio hatarini zaidi katika jamii
zetu. Kwa kufanya kazi na mashirika haya, tunaweza kusaidia juhudi
zinazoendelea ambazo zinalenga kushughulikia baadhi ya changamoto muhimu
zilizotokana na janga la COVID-19, "
Naye
Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Julius Kejo
amesema anaishukuru kwa msaada huo kwani utakwenda kunisaidia jamii
zinazokumbana na changamoto mbalimbali kutokana na janga la virusi vya
corona.
"fedha hizi
zitasaidia kushughulikia baadhi ya athari za haraka za kiafya na kijamii
zinazowakabili watu walio hatarini zaidi katika nchi yetu. Shukrani kwa
mchango muhimu kutoka kwa Standard Chartered, sasa tunaweza kuendelea
kusaidia watu zaidi wanaokabiliwa na athari mbaya za virusi vya corona. "
Mkurugenzi,
Idara ya Fedha ya Kibinafsi ya UNICEF na Ushirikiano, Gary Stahl
amesema "Tunashukuru kwa mchango huu kutoka Standard Chartered, UNICEF
itaweza kusaidia elimu ya mbali kupitia runinga, redio, simu za mkononi
na kufanya ulinzi kwa watoto walio katika mazingira hatarishi
ulimwenguni."
No comments:
Post a Comment