Na Tatu Mohamed
WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umepunguza idadi ya viambatanisho ambapo kwa sasa mtu anaweza kupata cheti chake akiwa na kiambatanisho kimoja muhimu.
Pia Rita imefanya punguzo la gharama za vyeti hivyo kutoka Sh.20,000 ya awali na kufikia Sh.10,000 kwa watu wazima huku watoto ikiwa ni Sh. 3,500.
Akizungumza katika banda lao lililopo katika maonesho ya 44 ya Biashara ya kimataifa ya Sabasaba, Ofisa Usajili Mwandamizi kutoka RITA, Hamisa Kileo amesema shughuli hiyo ya usajili iliyoanza hivi karibuni inaendelea ndani ya viwanja vya Sabasaba ambapo wamejipanga kuhakikisha kila mwananchi asiyekuwa na cheti hicho anamiliki.
"7RITA imejipanga vizuri kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wale wote ambao wamezaliwa Tanzania Bara lakini hawana cheti hicho hivyo tunawasihi wananchi hao wajitokeze kwa wingi katika banda la RITA lililopo hapa viwanja vya Sabasaba katika hema ya Jakaya Kikwete.
"Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu inayotumika katika nyanja mbalimbali katika mahitaji ya binadamu kama vile elimu, ajira, kupata mikopo ya elimu ya juu, bima ya afya, pasi ya kusafiria n.k. Hatahivyo cheti hiki kinaonesha utambulisho wa kwanza wa mwananchi mwenyewe kwa maana ya mahali alipozaliwa, majina ya mtoto, majina ya wazazi, tarehe ya kuzaliwa pamoja na ubini wa muhusika," amesema Hamida.
Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Rita Grace Kyasi amesema kuwa uwepo kwa huduma nyingi zinazohitaji mtu awe na cheti cha kuzaliwa imesababisha asilimia kubwa ya wananchi kuona kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na cheti hicho mapema hivyo kusababisha kuwepo kwa muitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza katika banda la RITA ili kupata huduma hiyo.
"Cheti cha kuzaliwa kimekuwa kikitumika kupata huduma mbalimbali kama vile kupata elimu ya msingi, sekondari, kupata huduma ya afya, kupata ajira katika taasisi za Serikali, jeshini na sekta binafsi. Hata hivyo cheti cha kuzaliwa humpa mtoto haki za kurithi mali za wazazi wake," amesema Grace.
Amesema mbali ya kutoa vyeti vya kuzaliwa RITA inatoa pia huduma ya msaada wa kisheria bila gharama yoyote kuhusu masuala ya kuandika na kuhifadhi wosia na mirathi pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya huduma zake nyingine kama vile ndoa na talaka, kuasili watoto pamoja na masuala ya udhamini.

No comments:
Post a Comment