Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Pwani Suzan Rymond akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya kazi zake ambazo wamezifanya kuanzia mwezi Aprili hadi juni mwaka 2020 pamoja na fedha ambazo wameweza kufanikiwa kuziokoa. (Picha na Victor Masangu).
VICTOR MASANGU, PWANI
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na
Rrushwa (TAKUKURU) imeokoa kiasi Cha Shilingi milion 35,000,000 kati ya milion
394,156335.30 ambazo ni fedha za malipo ya korosho kwa wakulima Mkoani Pwani.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani
Suzana Raymond alibainisha hayo jana wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya
Taasisi hiyo.
Alisema, Kampuni ya Mafubilo General
Supplies ya jijini Dar es salam iliyonunua korosho za wakulima kwa mkopo
kupitia Amcos za Visiga, Kongowe,Mwendapole,Mkombozi na Miembe saba zenye jumla
ya Shilingi milion 394,156,333.30.
Suzana alisema, malipo ya korosho
hizo yalisuasua hadi pale TAKUKURU ilipoinhilia Kati na kufuatilia
kuhakikisha mnunuzi analipa.
Mkuu huyo wa TAKUKURU alisema,
mdaiwa amepewa maagizo ya kulipa mpaka amalize deni lote haraka iwezekanavyo
ili wakulima wapate haki yao.
Katika hatua nyingine Taasisi hiyo
imeokoa Shilingi milion 4,900,000 za Mwalimu mstaafu Yusuph Kimweri ambaye
alikuwa amelipa kwa Ibrahim Masawe kupitia mkopo usiofuata kanuni taratibu na
sheria zinazosimamiwa na Taasisi za fedha nchini kiasi Cha Shilingi 700,000
aliokopa mwaka 2018.
Akiongelea suala hilo Suzana
alisema, kupitia riba deni lilikua na kufikia milion 13,000,000 ambalo Mstaafu
alilipa mara baada ya kupokea pensheni yake ya kustaafu Mei 27 2020.
Mkuu huyo wa TAKUKURU alisema, baada
ya kupokea malalamiko hayo walifanya uchunguzi wa kina na kubaini mtuhumiwa
alifanya biashara ya kukopesha fedha kinyume na kanuni .
Imeelezwa kuwa baada ya mtuhumiwa
kutambua kosa aliahidi kurejesha fedha hizo mpaka sasa amerejesha Shilingi
milion 4,900,000 na atatakiwa kukamilisha kiasi kilichobaki Cha Shilingi milion
8,100,000.
No comments:
Post a Comment