Na Denis Mlowe, Iringa
ZAIDI ya wanachama 250 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania
nafasi mbalimbali za uongozi katika majimbo na kata za uchaguzi wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa kwa siku mbili tangu kuanza rasmi utolewaji wa fomu kwa
Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na wanahabari Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi
James Mgego alisema kuwa wanachama wengi wamejitokeza tangu kuanza kutolewa
fomu za kuomba kuteuliwa siku ya jana kutokana na wengi wao kuwahiwa kuongoza
majimbo mbalimbali na kata katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa uwingi wa wachukua fomu ndani ya chama hicho ni
haki ya kila mwanachama anayetakiwa kuchagua au kuchaguliwa na kuonyesha ni
kiasi gani CCM wanademokrasia ya kweli ndani ya chama na wito wa huo imeonyesha
kuwa chama hicho kina viongozi wengi imara ambao wakichaguliwa watawaletea
maendeleo wananchi.
Mgego alisema kuwa wanachama wengi wamechukua fomu kwenye
ngazi ya kata ambao wanaomba kuteuliwa kuwa madiwani ambapo hadi kufikia leo
majira ya saa nne asubuhi wamekwisha jitokeza wanachama 119 ambapo wataongezeka
pindi mwisho wa kurudisha fomu za kura za maoni utakapokwisha.
Alisema kuwa kufikia leo wagombea wa nafasi za ubunge katika
majimbo ya Mufindi wamefikia idadi ya wachukua fomu 80 ambapo jimbo la Mufindi
Kusini limeonekana kuwa kinara kwa wagombea zaidi ya 24 kujitokeza ambapo siku
ya kwanza ya uchukuaji fomu walikuwa wachukua fomu 17 hali ambayo itaendelea
kwa wagombea kujitokeza zaidi.
Aliongeza kuwa jimbo la Mufindi Kaskazini wagombea
wamejitokeza kwa wingi ambapo idadi yao imefikia 17 na wanaendelea kujitokeza
kuchukua fomu jimbo ambalo lilikuwa chini ya mbunge Mahamud Mgimwa.
Kwa upande wa jimbo la Mafinga mjini wagombea waliojitokeza
kumpima alyekuwa mbunge wa jimbo hilo Cosato Chumi ni wagombea 9 ambapo wengi
wao walichukua fomu siku ya kwanza na wanatarajia kuongezeka hadi kufikia idadi
ya watia nia 15 hadi mwisho wa kurudisha fomu.
Mgego aliwataadharisha wagombea wote ambao wanamlengo wa
kutoa rushwa kwa wajumbe kuacha mara moja kwani chama kiko imara na mgombea
yoyote atakayebainika kufanya rafu kwenye kura za maoni chama hakitasita
kulikata jina lake na kuwataka kufanya yaliyondani ya kanuni na katiba za
chama.
Baadhi ya waliochukua fomu na kutaka kuteuliwa na
mwanahabari hizi kuwashuhudia ni, Ayoub Sanga, Marco Ng’umbi
(Mkalimoto),Modestus Kisoso John Malata na kwa upande wa udiwani wa viti maalum
Grace Mgina amechukua fomu za kutaka kuteuliwa.
No comments:
Post a Comment